Breaking News
recent

UEFA CHAMPIONS: ARSENAL, B.LEVERKUSEN, DORTMUND, REAL MADRID WATOKA KIFUA MBELE, JOGOO WA LONDON AFIA KWA MUUZA SUPU!!!



MSHAMBULIAJI Danny Welbeck amefunga hat trick yake ya kwanza Arsenal ikishinda 4-1 katika mchezo wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu Uwanja wa Emirates. Mshambuliaji huyo aliyenunuliwa kutoka
Manchester United msimu huu, alifunga magoli hayo katika dakika za 22, 30 na 52 wakati lingine
limefungwa na Alexis Sanchez dakika ya 41- huku bao la wageni likifungwa na Burak Yilmaz kwa penalti dakika ya 63. Kipa wa Arsenal, Szcezesny alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 60 na bado hiyo haikuizuia timu ya Arsene Wenger kushinda.


Mchezo mwingine wa Kundi D, Anderlecht imechapwa 3-0 nyumbani na Borrusia Dortmund, mabao ya Ciro Immobile dakika ya tatu na Adrian Ramos dakika ya 69 na 79.
Kundi A bao pekee la Ada Turan limetosha kuipa Atletico Madrid ushindi wa 1-0 dhidi ya Juventus wakati katika mchezo mwingine wa kundi hilo, Malmo FF ya Sweden imeichapa 2-0 Olympiacos ya Ugiriki mabao yake yakitiwa kimiani na M Rosenberg dakika ya 42 na 82.

Kundi B, Basel imeichapa 1-0 Liverpool bao pekee la Marco Streller dakika ya 52,majogoo hao wa london wamenywewa supu na hii ni mechi yao ya 3 kupoteza  wakati RealMadrid imeshinda ugenini mabao 2-1 dhidi ya PFC Ludogorets Razgrad. Wenyeji walitangulia kupata bao dakika ya sita kupitia kwa Marcelinho kabla ya Cristiano Ronaldo kufunga kwa penalti  dakika 25 na 77 karim benzema  kuipa bao la  ushindi, pia ronaldo alikosa penalti katika mchezo huo baada ya chicharito kufanyaniwa faulu eneo LA hatari.




Katika Kundi C, Zenit St Petersburg imetoka 0-0 na Monaco huku Bayer Leverkusen ikiitandika 3-1 Benfica, mabao ya Stefan Kiessling dakika ya 25, Heung-Min Son dakika ya 34 na Calhanoglu dakika ya 64, huku Eduardo Salvio akiwafungia Benfica dakika ya 62.

 


Waweza tazama matokeo kiurahisi Kwa kutazama chati ya matokeo hapa chini.




\
Unknown

Unknown

No comments:

Powered by Blogger.