Breaking News
recent

WAKALA WA CHRISTIANO RONALDO ATUMA SALAMU NZITO MAN UTD

CR7.Picha na footballwood.com
Wakala wa Christiano Ronaldo Jorge Mendes amesema mchezaji wake ana furaha Real Madrid na atabakia klabuni hapo kwa miaka kumi ijayo.

Mendes alisema hayo baada ya tetesi kuenea kuwa mkali huyo mwenye hat-trick 22 ana mpango wa kurudi Manchester United.

Wakala huyo aliongeza kuwa Ronaldo anaipenda United toka moyoni kwasababu ameishi kwa miaka 6 na ndio timu iliyouza jina lake lakini anafurahia kuwa Madrid na kila mtu anajua ni vigumu kumtoa CR7 Bernabeu.
Wakala huyo anaamini kuwa Ronaldo(30) ataendelea kuwa na kiwango cha juu mpaka atapofikisha miaka 40 ambapo toka ahamie Madrid mwaka 2009 amefunga magoli 269 kwenye mechi 257.

Pamoja na hayo wakala huyo linogesha kwa kusema zaidi ya kuwa mwanasoka bora Duniani ambaye hatatokea kwa miaka 500 ijayo lakini pia CR7 ni mwanariadha bora Duniani na hakuna wa kuweza kufananishwa nae.
Unknown

Unknown

No comments:

Powered by Blogger.