Breaking News
recent

SANOGO: MIAKA 3 ILIYOPITA NILIKUWA NALALA MITAANI

Akiwa bado hajaifungia goli klabu yake ya Arsenal, Yaya Sanogo amekuwa mtu wa kuchekwa na mashabiki wa klabu yake na timu pinzani, lakini hilo linaweza likawa sio jambo la haki, ukizingatia alivyopitia vizingiti vingi katika muda mfupi.
http://www.arsenal.com/assets/_files/scaled/794x500/jul_14/gun__1405066968_sanogo_profile1415.jpg
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 21 anayechezea timu ya vijana ya Ufatansa ameelezea kwa kina kuhus safari yake mpaka kufika hapo alipo katika mahojiano aliyofanya na mtandao rasmi wa Arsenal. – Arsenal.com, ambapo ndani ya mahojiano hayo anaeleza kwamba miaka mitatu iliyopita, alikuwa akiishi kwenye mitaa ya mji wa Auxerre huku akitafuta namna ya kupata nafasi ya kucheza kwenye ligue 1:
“Napata presha lakini watu wanatakiwa kutosahau kwamba, miaka mitatu iliyopita, nilikuwa naishi mitaani.>

“Leo naichezea klabu ya Arsenal.
“Nilipojiunga na Auxerre katika kambi yao ya mazoezi nilijua wazi kwamba nataka kuwa mchezaji mcheza soka na nilijiambia mwenyewe ni lazima niwe mchezaji bora. Nilisaini mkataba lakini nikaaumia kwa miaka miwili na baada ya kupona Arsenal wakanisajili.
“Magoli yatakuja lakini inabidi niendelee kucheza kwa bidii. Siku zote nina imani pale nitakapoanza kufunga sitoacha. Sijajipangia target bado, ninachojali zaidi ni kucheza zaidi na kukuza kiwango changu.
“Yes! Watu wataendelea kunipa presha – muda mwingine napata mawazo mazuri ya kunipa changamoto na muda mwingine pia wanakuwa wananionea, lakini naendelea kupambana na ninajiamini muda wangu utafika.”
Unknown

Unknown

No comments:

Powered by Blogger.