Breaking News
recent

HUYU KOCHA ALALAMIKA KUNYIMWA MWALIKO WA MVINYO NA VAN GAAL

thumbWakati wa utawala wa Sir Alex Ferguson katika klabu ya Manchester United alikuwa na utaratibu wa kuwaalika baadhi ya makocha wa timu pinzani kunywa mvinyo mara tu baada ya kumalizika kwa mchezo wowote katika dimba la Old Trafford.
Lakini chini ya utawala mpya wa kocha Louis Van Gaal utaratibu huo wa Ferguson umebadilika na tayari mmoja wa makocha waliokuwa wamezoeshwa na Fergie kualikwa kunywa mvinyo ametoa malalamiko yake.
Akiandika makala yake yaliyochapishwa kwenye gazeti la Evening Standard, kocha wa West Ham Sam Allardyce amesema ameshangazwa na kusikitishwa na kitendo cha kocha wa Manchester United Louis van Gaal kutomualika kunywa mvinyo baada ya mechi kati ya timu zao wikiendi iiyopita.
“Siku zote nilipokuwa nikienda Old Trafford nilikuwa nikialikwa kwa ajili ya mazungumzo kidogo pamoja na kunywa mvinyo.
“Huu utamaduni uliokuwepo kwa makocha wa timu pinzani, ndio maana nilishangazwa na kusikitishwa nilipotaarifiwa kwamba hakukuwa na utaratibu ule tena baada ya mechi kuisha. Niliambiwa utaratibu ule haupo tena, ikanibidi kuondoka.” - Aliandika Alladayce.
SOURCE: MILLARDAYO.COM
Unknown

Unknown

No comments:

Powered by Blogger.