Breaking News
recent

RONALDO AMPIKU MESSI KWA WALIOTAJWA ZAIDI MTANDAONI....ANGALIA TOP 10 HAPA


Mshambuliaji nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo au CR7 ameshika nafasi ya kwanza kuwa mwanamichezo anayetajwa zaidi mitandaoni.Ronaldo ameshika nafasi hiyo ya juu kwa kutajwa zaidi kwa mara 741,969.
Ronaldo amechukua nafasi hiyo baada ya kutajwa sana tokea Januari mwaka huu.
Nafasi ya pili imekwenda kwa mwanasoka mwingine, Lionel Messi ambaye ametajwa mara 599,115 na nafasi ya tatu ni mchezaji kikapu wa kikosi cha Miami Heat, LeBron James aliyetajwa mara 462,825.

Mchezaji tenisi Roger Federer ameshika nafasi ya nne akifuatiwa na mpinzani wake mkubwa Rafael Nadal.Nafasi ya sita na saba imekwenda kwa wacheza gpfu maarufu duniani Tiger Woods na Phil Mickelson.
Kwa makocha, aliyetajwa zaidi kwa kipindi hicho anaonekana ni Kocha wa Chelsea Jose Mourinho aliyetajwa mara 423,447.

Unknown

Unknown

No comments:

Powered by Blogger.