Breaking News
recent

FIFA YATOA ORODHA YA WACHEZAJI 23 WATAKAO WANIA BALLON D'OR 2014

Kwa mara nyingine tena Lionel Messi pamoja na Cristiano Ronaldo wanapambana katika harakati za kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka (FIFA Ballon d'Or) kufuatia majina yao kuonekana kwenye orodha iliyotolewa na shirikisho al soka duniani FIFA hii leo.
 Ni Ronaldo Na Messi Katika Tuzo Ya FIFA Ballon d
Wengine walioingia kwenye orodha hiyo ambao walipambana wakati wa kinyang’anyiro cha mchezaji bora wa mwaka 2013 ni mlinda mlango wa FC Bayern Munich pamoja na timu ya taifa ya Ujerumani Manuel Neuer, Neymar pamoja na Arjen Robben.
Kwa sasa tuzo hiyo inashikiliwa na Cristiano Ronaldo baada ya kumbwaga mpinzani wake wa karibu Lionel Messi wakati wa hafla ya kutangazwa kwa mchezaji bora wa mwaka 2013 iliyofanyika mwanzoni mwa mwaka huu.
Wawili hao wamewahi kutwaa tuzo ya mchezji bora zaidi ya mara moja ambapo kwa upande wa Lionel Messi aliwahi kuwa mshindi mwaka 2010, 2011 na 2012 ilihali Ronaldo alikuwa mshindi mwaka 2010 na 2013.
Katika orodha wa kuwania mchezaji bora wa mwaka 2014 klabu ya Real Madrid imeingiza majina ya wachezaji wake watano ambao ni Ronaldo, Bale, Karim Benzema, Toni Kroos, Sergio Ramos pamoja na James Rodriguez.
Upande wa FC Barcelona majina ya wachezaji wanne ambao ni Messi, Andres Iniesta, Javier Mascherano pamoja na Neymar.
Nao mabingwa wa soka nchini Ujerumani FC Barcelona wanawakilishwa na Mario Goetze, Philipp Lahm, Thomas Mueller, Arjen Robben, Bastian Schweinsteiger na mlinda mlango Manuel Neuer.
Klabu ya Chelsea inawakilishwa na mlinda mlango Thibaut Courtois, Diego Costa pamoja na Eden Hazard.
Klabu bingwa nchini UIngereza Manchester City inawakilishwa na Yaya Toure huku upande wa mahasimu wao Manchester United lipo jina la Angel Di Maria.
Kwa mabingwa wa soka nchini Ufaransa Paris Saint-Germain jina la mshambuliaji kutoka nchini Sweden Zlatan Ibrahimovic limejitokeza na kuwa mchezaji pekee wa klabu hiyo sanjari na kiungo Paul Pogba anaeitumikia klabu bingwa nchini Italia, Juventus.
Orodha kamili ya wachezaji wanaowani tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2014 iliyotolewa na FIFA.
Gareth Bale (Wales, Real Madrid), Karim Benzema (France, Real Madrid), Diego Costa (Spain, Chelsea), Thibaut Courtois (Belgium, Chelsea), Cristiano Ronaldo (Portugal, Real Madrid), Angel Di Maria (Argentina, Manchester United), Mario Goetze (Germany, Bayern Munich), Eden Hazard (Belgium, Chelsea), Zlatan Ibrahimovic (Sweden, Paris Saint Germain), Andres Iniesta (Spain, Barcelona), Toni Kroos (Germany, Real Madrid), Philipp Lahm (Germany, Bayern Munich), Javier Mascherano (Argentina, Barcelona), Lionel Messi (Argentina, Barcelona), Thomas Mueller (Germany, Bayern Munich), Manuel Neuer (Germany, Bayern Munich), Neymar (Brazil, Barcelona), Paul Pogba (France, Juventus), Sergio Ramos (Spain, Real Madrid), Arjen Robben (Holland, Bayern Munich), James Rodriguez (Colombia, Real Madrid), Bastian Schweinsteiger (Germany, Bayern Munich) pamoja na Yaya Toure (Ivory Coast, Manchester City)
Wakati huo huo FIFA wametoa orodha ya makocha wanaowani tuzo ya kocha bora wa mwaka.
Carlo Ancelotti (Real Madrid), Antonio Conte (Juventus/Italy), Pep Guardiola (Bayern Munich), Juergen Klinsmann (USA), Joachim Loew (Germany), Jose Mourinho (Chelsea), Manuel Pellegrini (Manchester City), Alejandro Sabella (Argentina), Diego Simeone (Atletico Madrid) pamoja na Louis van Gaal (Holland/Manchester United)
Unknown

Unknown

No comments:

Powered by Blogger.