Breaking News
recent

JINSI YA KUINSTALL WHATSAPP KWENYE JAVA PHONES KAMA NOKIA ASHA 200 NA 205

Habari za leo wapendwa, leo ningependa kuwapa somo linalohusiana na kutumia whatsapp kwenye simu aina ya nokia asha 200 na 205 (simu pichani hapo chini)


Tafadhari hii ni muhimu sana, unatakiwa uwe na nafasi katikasimu yako (internal space) at least iwe 5mb na hii ni muhimu zaidi, hizi simu ni za laini mbili kwahiyo unatakiwa uweke laini zote ili wakati wa kuinstall na kufanya setting isikusumbue....

FUATA HATUA ZIFUATAZO KWA MAKINI

1) Download raw file kutoka HAPA na hili ni zipped file..

2) Li unzip hilo file ulilolidownload, halafu licopy folder zima kwenye memory card (Hii unatakiwa ufanyie computer, halafu hilo folder weka kwenye memory card kisha toa weka kwenye simu)

3) Sasa nenda kwenye hilo folder ndani ya simu ila usilifungue kwanza

4) Copy application hiyo kutoka kwenye memory card kwenda kwenye memory ya simu ( my apps au games)

5) Sasa rudi katika folder kule kwenye memory card na ulifute kabisa...

6) Ukimaliza nenda katika application yako ya whatsapp kwenye simu, bonyeza kitufe cha OPTION  na bonyeza UPDATE VERSION, iache iupdate ikimaliza ifungue hiyo apps... Sasa waweza fuata maelekezo yanayoendelea, ikifunguka kabisa utapata UPDATE NOTIFICATION ENABLER iache iendelee kusoma, itakataa na kukwambia NOT SUPPORTED, ifunge na whatsapp yako itakuwa imeinstall na inafanya kazi vizuri... 

USIACHE KUCOMMENT HAPO CHINI KAMA UMESHINDWA AU UMEFANIKISHA, PIA SHARE NA WENZAKO WAWEZE KUJUA

MUHIMU: FILE LINADOWNLOAD KUPITIA KWENYE COMPUTER KISHA COPY FILE KWENYE MEMORY CARD NA HUAMISHIE MEMORY KWENYE SIMU....
Unknown

Unknown

No comments:

Powered by Blogger.