Breaking News
recent

DI MARIA AWA MCHEZAJI BORA WA MWEZI MAN UNITED,

WINGA Angel di Maria amepata malipo hya kazi yake nzuri Septemba baada ya kupewa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa klabu hiyo kwa mwezi huo Manchester United. Mchezaji aliyesajiliwa kwa dau la rekodi katika klabu hiyo msimu huu tayari amekuwa tegemeo la kocha Louis van Gaal Old Trafford na alishinda kwa kishindo tuzo hiyo, akipata asilimia 68 ya kura. Ander Herrera na Rafael walipata asilimia 23 na asiimia tisa ya kura, lakini nyota huyo wa Argentina ameshinda kura zilizopigwa kwenye tovuti ya klabu hiyo, ManUtd.com. Angel Di Maria amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Septemba Manchester United akimshinda Herrera Di Maria alifungua akaunti yake ya mabao Manchester United katika mechi dhidi ya QPR, kabla ya kufunga bao la mapema la msimu dhidi ya Leicester "Nina furaha sana kupokea tuzo hii, lakini sijavutiwa na mwenendo wa timu," Di Maria ameiambia ManUtd.com "Nina furaha kwamba nimeanza vizuri kazi yangu Manchester United, na ninatumaini ninachokifanya uwanjani ni kuisaidia timu kupata pointi na kuchukua ushindi,"amesema.

Unknown

Unknown

No comments:

Powered by Blogger.