Breaking News
recent

WATOTO WAWILI WAPIGWA, WAZOMEWA NA KUITWA JINA LA EBOLA HUKO NCHINI MAREKANI...SOMA KISA!!!



Watoto wawili wa kiume wenye umri wa miaka 11 na 13 wameshushiwa makonde wanafunzi
wenzao na kuwaita jina la ?Ebola?. Watoto hao wawili raia wa Senegal walihamia
Marekani mwezi mmoja uliopita? waliporomoshewa kipigo? wakiwa shuleni I.S
318, New York katika viwanja vya michezo ambapo wenzao waligoma kushiriki nao
michezo na kwa kile walichodai wataambukizwa Ebola na baadaye kuwazonga
na kuwapiga. Taarifa zinasema baba wa watoto hao, Ousame Drame amekuwa akipewa taarifa na
watoto wake kuwa tangu wafike shuleni hapo wamekuwa wakinyanyapaliwa kwa kuitwa
Ebola, kitu ambacho kimekuwa kikiwakasirisha na kumtaka baba yao awarudishe Senegal.
Idara ya Elimu New York imethibitisha kupokea taarifa zinazohusu vijana hao.
Baba huyo amesema japo watoto hao wamekulia Senegal lakini wana haki za kuishi
Marekani kwa kuwa walizaliwa huko, na moja ya matatizo linalowakabili ni kutokujua lugha
ya kiingereza kutokana na kukulia nchini Senegal ambako inazungumzwa lugha ya Kifaransa.
Unknown

Unknown

No comments:

Powered by Blogger.