MSHAMBULIAJI Luis Suarez ameichezea tena kwa mara ya kwanza Uruguay baada ya miezi minne ya kutumikia adhabu ya FIFA kwa kumng'ata begani Giorgio Chiellini wa Italia- kufuatia kuiongoza Uruguay kupata sare ya ugenini 1-1 na Saudi Arabia. Mshambuliaji huyo mpya wa Barcelona mwenye umri wa miaka 27, alipiga shut zuri la mpira wa adhabu ambalo liligongwa mwamba kabla ya beki Hassan Muath Fallatah kujifunga dakika ya 47. Hata hivyo, bao la Suarez ambaye alipunguziwa adhabu na Mahakama ya Usuluhishi ya FIFA (CAS) na kuruhusiwa kucheza mechi zisizo za mashindano, bao lake halikudumu kufuatia Naif Hazazi aliyetokea benchi kuisawazishia Saudi Arabia dakika ya mwisho. Amerudi;
Luis Suarez akipongezwa na wenzake jana baada ya kusababisha bao la kuongoza la Uruguay Baada ya mechi, mchezaji huyo aliyehamia Barcelona kutoka Liverpool msimu huu kwa dau la Pauni Milioni 75, alisema: "Furaha kuvaa jezi hii tena ambayo inanipa mimi raha mno. Huwei kupoteza mapenzi yako kwa jezi. Uruguay!' Suarez, ambaye katikati ya mchezo aliomba ruhusa kwenda chooni mara moja na akakubaliwa na refa, kwa ujumla alicheza vizuri kwenye mchezo huo kabla ya kumpisha mwenzake dakika ya 70. |
No comments:
Post a Comment