Breaking News
recent

CHEKI PICHA NA VIDEO EPL: CHELSEA YAIUA ARSENAL, COSTA KAMA KAWAIDA YAKE, HUKU MANUTD WAKIONDOKA KWA KICHEKO, MATOKEO YOTE YAPO HAPA

IMG_7773.PNG
Ile mechi ya kuamua nani mbabe wa jiji la London kati ya Chelsea dhidi ya Arsenal imemalizika muda mfupi uliopita.
Matokeo kwenye mchezo huo uliokuwa na kashi kashi nyingi ukiwemo ugomvi wa kushikana mashati wa Wenger dhidi ya Mourinho – ni ushindi wa 2-0 kwa Chelsea.
Eden Hazard alianza kuiadhibu Arsenal kipindi cha kwanza baada ya kufunga mkwaju wa penati baada ya kufanyiwa madhambi na Koscienly.
Kipindi cha pili katika dakika za mwishoni Diego Costa alipokea pasi nzuri kutoka kwa Cesc Fabregas na akaifungia Chelsea goli la pili na kuhitimisha ushindi huo dhidi ya Gunners.



Baada ya kukubali kunyanyashwa mara mbili mfululizo msimu uliopita na Everton, hatimaye leo Manchester United ilipata nafasi kufuta uteja wao kwa klabu hiyo ya Merseysed.
Katika mchezo uliomalizika hivi punde katika uwanja wa Old Trafford umemalizika kwa Man United kufuta uteja mbele ya Everton.

IMG_7752.JPG

Kikosi cha Louis Van Gaal kimefanikiwa kupata ushindi wa 2-1.
Angel Di Maria alifungua akaunti ya magoli katika mchezo wa leo katika dakika ya 25 baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Juan Mata.
Dakika moja kabla ya mapumziko Leighton Baines alikosa mkwaju wa penati baada ya Luke Shaw kumkwatua mchezaji wa Everton.
Kipindi cha pili Everton walirudi vizuri na kufanikiwa kupata goli la kusawazisha kupitia Naismith.
Baada ya goli hilo Man United wakajipanga upya na alikuwa yule yule Angel Di Maria akatoa pasi nyingine ya mwisho kwa Falcao aliyefunga goli la ushindi.
United inabidi wamshukuru kipa David De Gea kwa kazi nzuri aliyoifanya kuokoa michomo ya magoli ya wazi na hatimaye wakafanikiwa kumaliza mchezo wakiwa na ushindi wa 2-1.
MATOKEO YOTE HAYA HAPA:

Manchester United2 - 1Everton

Tottenham Hotspur1 - 0Southampton

Chelsea2 - 0Arsenal

West Ham United2 - 0Queens Park Rangers




Unknown

Unknown

No comments:

Powered by Blogger.