HILI NI JENEZA LA AINA YAKE: MZEE MMOJA NCHINI KENYA AZIKWA KATIKA JENEZA AKIWA AMEKAA
Kuna taarifa ambazo kama ukibahatika zikakufikia, zinaweza kukuacha kinywa wazi ama
kukushtua kwa namna fulani. Stori ambayo nimeipata hivi punde kutoka 254
Kenya inahusiana na mazishi ya aina yake ambapo familia moja imefanya mazishi ya mzee
wao aliyekuwa akifahamika kwa jina la Adriano Aluchio anayetajwa kuwa mzee wa kuheshimika
kwenye jamii hiyo akiwa amekaa ndani ya jeneza lilichongwa kwa namna ya kipekee tofauti
na ilivyozoeleka. Baadhi ya watu waliohojiwa kuhusiana na tukio
hilo wamesema ni utamaduni wa jamii ya kabila la Lughia kufanya mazishi ya namna hiyo kwa
mzee aliyeheshimika, kwa imani kuwa amefariki lakini anaendelea kuwalinda watoto wake
pamoja na jamii yake. Moja ya wazee katika jamii hiyo amenukuliwa
akisema, ?Mazishi kama hayo ya kumkalisha marehemu yalianza tangu zamani sana wakati
wa mfalme Nabongo Mumia, na sisi tulitokea katika jamii hiyo, tukimzika amelala
hatoridhika? Ataonekana akitembea huku juu?.? Baada ya mazishi hayo ya kipekee,
walichukuliwa ng?ombe dume wawili na kupiganishwa juu ya kaburi kama njia ya
kufukuza mapepo wachafu, huku wanakijiji wakipongeza kitendo cha mzee huyo kupewa
mazishi ya hadhi. Jamii ya Waidakho katika kabila la Walughia
wanoishi katika kaonti ya kakamega wanajulikana sana kwa mchezo wao
unaowavutia watalii eneo hilo la kuwapiganisha Fahali na kuku Jogoo.
No comments:
Post a Comment