PINA ATOA SABABU ZA KUMPIGA CHIDI BENZ
"Ukweli ni mambo ya
fedheha, mdogo wetu Chidi Benz, nnacho weza kusema mdogo wetu ni kwamba unga
anaovuta sasa hivi unampeleka pabaya umeona eeh, tena mimi kama kaka yake
namshauri aachane na matumizi ya madawa ya kulevya kwasababu mwisho wake
utampeleka pabaya, mimi niko back stage nna show yangu nipo kazini, tupo seious
watu wa hiphop, miaka mingi tulikuwa tuna nadi amani hatutaki matatizo na watu
unaona bana, hawa ni watu ambao kwa namna moja ama nyingine wanasababisha hiphop
ishindwe kwenda mbele na kusababisha hiphop ishindwe kwenda mbele na kuwapa
mafanikio watu wa hiphop.tumeandaa show yetu nzuri, ilikua bonge ya show moja
kali ya hiphop Tanzania kuwahi kutokea, show ambayo imekutanisha wasanii wakali
wa hiphop ambao sasa hivi wanavuma, mi niko back stage naskia sauti ya Chidi
Benz ameshika mic, muda ambao mi natakiwa kuwa stage naperfom, sa Chidi Benz
ametokea wapi mbona kwenye ratiba yetu ya show hayupo, anaongea ubabe
anakamba.yupo stage mi niko back stage bado, mi nikawaambia watu wangu vipi,
huyu mtu mbona mnamuachia anatuharibia show? hasa watu ujue, ujue msanii, yaani
jana ndio nimekubali msanii ni mtu mwenye hadhi na heshima kubwa sana sema Chidi
Benzi amejishushia hadhi yake na heshima yake .Watu wakawa wanashindwa kumfanya
kitu wakiangalia huyu ni mtu maarufu anajulikana, watu wakawa wanamplease
kiustaarabu, Chidi eeh shuka hii show haikuhusu, sasa watu walivyokuwa
wanamplease akawa anaona labda watu mafala au nini umeona eeh.
sasa mimi kitendo
kimechukua kama dakika saba au nane hivi, bado yuko tu stage ameng'ang'ania,
ananichelewesha mimi muda wa kuperfom, watu wanataka kuona show yangu, watu
wamelipa hela zao, wameacha shughuli zao waje kumuona kalapina, ye anataka
kuzkwaza watu wasimuone Kala pinia, huyu mtoto si adui jamani......." amesema
Kala Pina ..
No comments:
Post a Comment