Breaking News
recent
RIO AMUAGA SIR ALEX KWA BAO SAFIII LA USHINDI!!

>>SIR ALEX FERGUSON RASMI AAGA OLD TRAFFORD!!
>>SCHOLES NAE AAGWA!!
>>MABINGWA MAN UNITED RASMI WAPEWA TAJI, MEDALI ZAO!!
SIR_ALEX_FERGUSON-LAST_OLD_TRAFFORDMABINGWA MANCHESTER UNITED LEO WAKIWA KWENYE SIKU YA KIHISTORIA YA KUMUAGA MENEJA WAO SIR ALEX FERGUSON BAADA YA UTUMISHI WA MIAKA 27 kwenye Mechi yao ya mwisho ya Msimu huu wa BPL, Barclays Premier League, kuchezwa Uwanjani kwao Old Trafford walipocheza na Swansea City na pia kukabidhiwa rasmi Kombe lao la Ubingwa, walishinda Mechi hii kwa Bao la Dakika ya 87 la Rio Ferdinand hilo likiwa Bao lake la kwanza baada ya Miaka mitano.
++++++++++++++++++++
MAGOLI:
Man United 2
-Chicharito Dakika ya 39
-Rio 87
Swansea 1
-Michu Dakika ya 49
++++++++++++++++++++
Kabla ya Mechi kuanza, Wachezaji wote wa pande mbili, Man United na Swansea City, walimuwekea Sir Alex Ferguson Gwaride la Mistari miwili kumpa hashima.
Na maara baada ya Mechi kwisha, na kabla Manchester United kukabidhiwa Kombe lao la Ubingwa wa BPL, Sir Alex Ferguson alitoa Hotuba.
++++++++++++++++++++
BAADHI DONDOO MUHIMU ZA SIR ALEX:
-AMESHINDA MECHI 514 KATI YA 723 WALIZOCHEZA OLD TRAFFORD
-AMETWAA MAKOMBE 38, AKITWAA KOMBE 1 KATIKA KILA MSIMU KATIKA MISIMU 19 KATI YA 24 ILIYOPITA
-AKIWA MAN UNITED, AMETUMIA JUMLA YA WACHEZAJI 209
++++++++++++++++++++
Kwenye Hotuba yake, Sir Alex Ferguson, aliiambia Old Trafford sasa kazi yao ni kumpa sapoti Meneja mpya David Moyes.
VIKOSI:
Man United: De Gea, Jones, Vidic, Ferdinand, Evra, Carrick, Scholes, Welbeck, Kagawa, Van Persie, Hernandez.
Akiba: Lindegaard, Evans, Buttner, Abderson, Valencia, Cleverley, Giggs
Swansea City: Tremmel, Tiendalli, Chico, Williams, Taylor, Britton, de Guzman, Routledge, Hernandez, Dyer, Michu
Akiba: Cornell, Monk, Rangel, Davies, Agustien, Shechter, Lamah.
Refa: Jon Moss
BPL: BARCLAYS PREMIER LEAGUE
RATIBA
Jumanne Mei 14
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
Arsenal v Wigan
[Saa 4 Usiku]
Reading v Man City
Jumapili 19 Mei
***MECHI ZA MWISHO ZA LIGI MSIMU HUU
[Saa 12 Jioni]
Chelsea v Everton
Liverpool v QPR
Man City v Norwich
Newcastle v Arsenal
Southampton v Stoke
Swansea v Fulham
Tottenham v Sunderland
West Brom v Man United
West Ham v Reading
Wigan v Aston Villa
+++++++++++++++++++++++
Unknown

Unknown

No comments:

Powered by Blogger.