TAARIFA ZA AWALI KUHUSU MFANYABIASHARA ALIYEJIRUSHA TOKA GHOROFA YA TISA KARIAKOO
TAARIFA za awali zina arifu
kuwa Mfanya Biashara, Costa Shirima anaedaiwa kujirusha kutoka gorofa ya tisa ya
Hoteli ya Concord iliyopo Kariakoo Jijini Dar es Salaam inaelezwa kuwa alifariki dunia muda mfupi baada ya
kujirusha na alikuwa asafiri na ndege ya saa 10 jioni kuelekea China kufuata
bidhaa za maduka yake.
Shirima (47), ambaye amefikwa
na umauti muda mfupi baada ya kudondoka chini ni mfanyabiashara aliyekuwa
akimiliki maduka kadhaa ya urembo wa akina mama yaliyopo jirani na Hoteli hiyo
ya Concord.
Aidha taarifa hizo za awali
kutoka kwa mmoja wa wanafamilia ambaye alidai kuwa si msemaji wa familia ya
Shirima ya Mwika Moshi mkoani Kilimanjaro, nikuwa Marehemu mara kwamara alikuwa
akipendelea kula katika hoteli hiyo na siku ya tukio inadaiwa kuwa aliwaeleza
watu kuwa anapanda juu ya Hoteli hiyo kupunga upepo baada ya kuhisi hewa nzito
mahali alipokuwa.
Inadaiwa kuwa baada ya kupanda
huko juu ghafla alianguka chini na kudondokea gari dogo aina ya Toyota Corola
linalofanya biashara ya Taxi na kupoteza maisha yake na gari hilo kuharibika
vibaya kutokana na kishindo hicho.
Marehemu Shirima mbali na kuwa
Mfanya Biashara wa muda mrefu Kariakoo pia alikuwa akiendelea na Ujenzi wa Jengo
la Gorofa maeneo ya Kariakoo.
Marehemu ameacha Mjane na
watoto 5.
No comments:
Post a Comment