HII NDIO NCHI NGUMU ZAIDI DUNIANI KULEA WATOTO
Shirika
la Save the Children, limeeleza kuwa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)
kuwa ndio nchi ngumu zaidi duniani kulea watoto.
Nchi
ya Finland imetajwa kuwa sehemu bora duniani kuwa mama, huku Sweden na Norway
zikifuatia katika nafasi ya pili na tatu.
Shirika
hilo la hisani limetumia vigezo vya huduma ya afya kwa akina mama, vifo vya
watoto, elimu na kipato katika nchi 186 duniani kutoa takwimu hizo.
Nchini
India, zaidi ya watoto 300,000 hufariki dunia saa 24 baada ya kuzaliwa, hivyo
kuchangia 29% ya vifo vya watoto wanaozaliwa duniani kote imeeleza ripoti ya
shirika hilo.
Nchi
kumi zilizoshika nafasi ya mwisho zote zinatoka eneo la Kusini mwa Jangwa la
Sahara, ambako kwa wastani, mwanamke mmoja katika 30 hufariki dunia kutokana na
matatizo ya ujauzito na mtoto mmoja kati ya saba hufariki kabla ama baada ya
kufikisha umri wa miaka mitano.
Nchini
DRC, vita na umasikini vimewaacha akina mama wakiwa dhoofu kiafya na bila msaada
wowote hasa wakati wa hatari kubwa katika maisha yao.
Nchi
nyingine zilizotajwa kuwa hatari ni Somalia, Sierra Leone, mali, Niger, Jamhuri
ya Afrika ya Kati, Gambia, Nigeria, Chad na Cote D’Ivoire.
Shirika
hilo la hisani limesema, ukosefu wa lishe bora ni sababu kubwa ya kuongezeka kwa
idadi ya vifo vya akina mama na watoto wachanga katika nchi za Kusini mwa Jangwa
la Sahara, huku 10% - 20% ya akina mama wakiwa hawana uzito unaostahili.
Kinyume
chake, matokeo hayo yanaonesha kuwa, Finland ni nchi bora kuwa mama, huku hatari
za vifo vitokanavyo na ujauzito ikiwa ni moja kati ya akina mama 12,200 na
watoto katika nchi hiyo wakihudhuria karibu miaka yote 17 ya elimu ya
awali.
Sweden,
Norway, Iceland na Uholanzi zilikuwa pia miongoni mwa nchi bora 10, ambapo
Marekani iko nyuma katika nafasi ya 30.
Lakini
jambo la kustaajabisha, ripoti ya shirika hilo imebaini kuwa, Marekani ina
kiwango cha juu cha vifo vya watoto wanaozaliwa katika nchi zenye viwanda
duniani, ambapo watoto 11,300 hufariki dunia katika siku wanayozaliwa kila
mwaka.
Shirika
hilo limesema, hali hiyo inasababishwa na idadi kubwa ya watu nchini Marekani
pamoja na wingi wa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati. Marekani ni miongoni mwa
nchi zenye kiwango cha juu cha watoto wanaozaliwa kabla ya wakati ikiwa na
uwiano wa mtoto mmoja kati ya wanane.
Ipoti
hiyo imegundua kuwa, akina mama na watoto hufariki dunia kwa idadi kubwa huko
Kusini mwa Asia kuliko eneo lolote duniani, ikikadiriwa kuwa, watoto 423,000
hufariki dunia siku wanayozaliwa kila mwaka.
India
imetajwa kuwa na idadi kubwa ya vifo vya watoto wachanga,(ikiwa ni 29% ya vifo
duniani) na pia vifo vingi vya akina mama kuliko nchi yoyote duniani ambapo
akina mama 56,000 hufariki kila mwaka.habari kutoka BBC
No comments:
Post a Comment