Breaking News
recent
                             SPICHI YA SIR ALEX FERGUSON OLD TRAFFORD

>>ASEMA: “MLINISAIDIA, SASA SIMAMENI KWA MENEJA MPYA”
>>KWA WACHEZAJI: “MNAJUA NYINYI NI WAZURI, MNAIJUA JEZI MNAYOIVAA, NA MNAJUA NINI UMUHIMU WAKE KWA KILA MTU HAPA.”
>>AAGA: “NAKWENDA NYUMBANI, NAKWENDA NDANI KWA MUDA.”
MAN_UNITED-2013-TROPHYJUMAPILI MEI 12, ILIKUWA NI MECHI YA 1499 YA SIR ALEX FERGUSON AKIWA MENEJA WA MANCHESTER UNITED, NA ALIKUWA AKIAGA RASMI KWENYE MECHI YAKE YA MWISHO UWANJANI OLD TRAFFORD AMBAPO PIA WALIKABIDHIWA KOMBE LAO LA UBINGWA, BAADA YA KUTANGAZA KUSTAAFU KUFUATIA UTUMISHI WA MIAKA 27.
KABLA KUKABIDHIWA KOMBE LA UBINGWA, SIR ALEX FERGUSON, ALIHUTUBIA:
“Sina Hotuba rasmi akilini mwangu, nitaanza tu kubwabwaja nikitegemea nitafika kwenye misingi ya nini Klabu hii inatakiwa kuwa.
Kwanza kabisa, ni asanteni sana kwa Manchester United, sio pekee Wakurugenzi, Madaktari, Makocha, Wachezaji, Mashabiki, ni nyinyi nyote. Nyinyi wote mmekuwa bora katika maisha yangu.
Asanteni sana.
Nimebahatika sana.
Nimeweza kuwa Meneja wa Wachezaji Bora Nchi hii ukiachilia mbali Manchester United.
Wachezaji wote hawa wameiwakilisha Klabu yetu kwa njia sahihi na wametwaa Ubingwa kwa fasheni safi sana.
Hongera kwa Wachezaji.
Kustaafu kwangu hakumaanishi ndio mwisho wa maisha yangu kwa Klabu.
Sasa nitapata raha ya kuwaangalia badala ya kuumia na wao.
Ukifikiria hilo, Magoli ya Dakika ya mwisho, kuibuka toka nyuma tukiwa tumefungwa magoli na kushinda na hata kufungwa ni sehemu ya hii Klabu yetu kubwa.
Ni maisha ambayo huwezi kuyaamini, kwa hiyo asanteni nyote.
Nataka pia niwakumbushe kuwa wakati wote tukiwa kwenye hali mbaya Klabu ilinipa sapoti, Wafanyakazi wote walikuwa kwangu, Wachezaji walikuwa kwangu, wote walinipa sapoti—kazi yenu sasa ni kusimama kwa Meneja mpya.SIR_ALEX_FERGUSON_NA_GRANDAD_TEAM_OF_11
Hilo ni muhimu.
Kabla sijaanza kusema ovyo, napenda kutoa pongezi za dhati kwa Paul Scholes ambae leo anastaafu.
Huwezi kuamini yeye ni mmoja wa Wachezaji Bora wa Klabu hii ambao wamepata kuonekana au wataonekana.
Paul, tunakutakia mapumziko mema. Najua utakuwepo ili uendelee kunikera.
Pia, napenda kusema kidogo kuhusu Darren Fletcher kumtakia apone haraka.
Kwa Wachezaji, nawatakia mafanikio mema hapo baadae.
Mnajua nyinyi ni wazuri, mnaijua Jezi mnayoivaa, na mnajua nini umuhimu wake kwa kila Mtu hapa.
Msijiangushe wenyewe, hapa matumaini daima yapo.
Nakwenda nyumbani, nakwenda ndani kwa muda.
Nataka kuwashukuru nyote toka kwa Familia ya Ferguson, wote wapo hapa-Wajukuu 11.
Asanteni, Asanteni”
Unknown

Unknown

No comments:

Powered by Blogger.