RAISI JAKAYA KIKWETE AKATISHA ZIARA NCHINI KUWAIT NA KURUDI BONGO
Raisi Jakaya Mrisho Kikwete,
amekatisha ziara yake ya kikazi nchini Kuwait na anatarajiwa kurudi jijini Dar
es salaam, ili kushughulikia tukio la kulipuliwa kwa kanisa la Mtakatifu Yoseph
Mfanyakazi Olasiti jijini Arusha, lililokuwa lizinduliwe jana na balozi wa
Vatican nchini Tanzania Askofu Francis Kadinda.
Akizungumza na Clouds Fm
kutokea nchini Kuwait, Mkurugenzi wa kurugenzi ya mawasiliano ya Raisi Ikulu,
Salva Rweyemamu amesema, Raisi amepata taarifa hizo mara baada ya kutua nchini
humo jana na kusikitishwa na kitendo hicho alichokitaja kutaka kuvuruga amani na
usalama wa Tanzania na watu wake.
Tukio hilo lililotokea jana
jijini humo limesababisha mtu mmoja kuuwawa na wengine zaidi ya 40
kujeruhiwa
No comments:
Post a Comment