Breaking News
recent

VIDEO: MJUE KIUNGO WA REAL MADRID ALICHOFANYIWA NA MASHABIKI WAKE...

Gareth Bale Real MadridMashabiki wa soka wanapofungwa mara nyingi huchukulia jazba kutokana na matokeo mabaya waliyopata na wakati mwingine hufikia hatua ya kufanya vurugu ikiwa tu ni kutokana na matokeo mabaya waliyoyapata.
Hii ilitokea kwa mashabiki wa Real Madrid ambao walipandwa na jazba na kuamua kulivamia gari aina ya Bentley lililokuwa linaendeshwa na kiungo Gareth Bale na kulipiga mateke na ngumi kufuatia matokeo mabaya kwa timu hiyo.
Mashabiki hao walikuwa wanamsubiri mchezaji huyo njiani kwa hamu ya kumvaa wakidai wamefikia hatua hiyo baada ya Bale kushindwa kuisaidia timu hiyo wakati ikicheza na Barcelona na kupoteza mchezo huo kwa jumla ya mabao 2-1 kwenye Uwanja Camp Nou.
Inasemekana pamoja na hasira ya kufungwa lakini pia wamekuwa na chuki ya muda mrefu na kiungo huyo huku wakiusgutumu uongozi wa klabu hiyo kwa kumnunua kwa gharama kubwa kutoka Tottenham.
Hata hivyo uongozi wa Real Madrid umewafungia mashabiki wote waliohusika kwenye tukio la kumshambulia mchezaji huyo.

Unknown

Unknown

No comments:

Powered by Blogger.