Kwenye story ambazo zinahusu matukio ya kushtua na kushangaza kwa upande mwingine ni hii ya jamaa ambaye aligoma kushuka kwenye ndege baada ya ndege hiyo kutua, story ikazidi uukubwa baada ya jamaa huyo kwenda kujificha katika chumba ambacho wanakaa marubani.
Maofisa wa usalama wa Uwanja wa ndege New York walitumia nguvu kumtoa jamaa huyo ambaye anaishi New Jersey , muda wote aligoma kushuka kwenye ndege akidai kwamba kuna kundi la watu walikuwa wanataka kumdhuru.
Baada ya kutolewa alipelekwa Hospitali ya Jamaica ili kumcheki kama ana tatizo lolote la akili huku wakimfungulia mashitaka kwa kufanya kosa hilo.
Ndege hiyo ilitua New York ikitokea Jamhuri ya Dominica.
No comments:
Post a Comment