Chelsea licha ya kuwa katika harakati za kutaka kuutwaa ubingwa wa ligi kuu ya England msimu huu pia iko katika kuhakikisha inakisuka upya kikosi chake na sasa imedhamiria kumnyakua kiungo wa Real Madrid, Gareth Bale.
Iwapo itakubaliana na Real Madrid klabu hiyo tayari imetenga kiasi cha pauni milioni 75 ikiwa ni rekodi mpya ya usajili.
Iwapo itakubaliana na Real Madrid kumnasa Bale kwa kitita hicho itakuwa ni rekodi mpya ya usajili nchini England.
Taarifa ya gazeti la Dailymail la Uingereza zimeeleza kuwa Real Madrid tayari wana taarifa hizo za Chelsea lakini bado hawana mpango wa kumtoa mchezaji huyo na wanataka angalau Bale abaki msimu mmoja zaidi.
Bale alitua Madrid kwa kitita cha pauni milioni 86 akitokea Tottenham na kumfanya awe mchezaji ghali zaidi duniani.
Raia huyo wa Wales, tayari ameanza kuonyesha cheche zake akiwa na Madrid na jana aliifungia timu yake ya taifa mabao mawili wakati ikiichapa Esrael kwa mabao 3-0 katika mechi ya kuwania kucheza michuano ya Ulaya.
No comments:
Post a Comment