Unajua hii imekuwa ishu ambayo inakaa
sana kwenye headlines, upande wa Bongo Sheria zimebanwa zaidi kuzuia
matumizi ya dawa za kulevya, Marekani tukasikia story tofauti, wao kuna
Majimbo ambayo yaliruhusu matumizi ya Bangi, uhalali huu umeingiza Bangi
kuwa bidhaa halali kabisa kutumiwa na kuuzwa kama ilivyo bidhaa
nyingine Majimbo kama ya Washington DC, Alaska, Colorado.
Hii ya leo ni kwamba Jimbo la Colorado
unaambiwa wamefanikiwa kukusanya kodi ambayo ni dola Mil. 15 (zaidi ya
Bil. 27 Tshs) kutokana na mauzo ya bangi ndani ya kipindi cha mwaka
mmoja.
Fungu hilo la kodi linapelekwa kujenga Shule mbalimbali kupitia mpango wa Jimbo hilo uliopewa jina la Building Excellent Schools Today (BEST)
Tangu kupitishwa utaratibu wa kuruhusu
uuzaji wa bangi, unaambiwa maduka ya kuuza bidhaa hiyo rejareja mtaani
kuanzia Jan. 1, 2014 mpaka sasa wamefanikiwa kufanya mauzo na kulipa
kodi ambayo ni kama dola Mil. 15 ambazo zinasaidia ujenzi wa Shule za
Umma katika Jimbo hilo.
Kwako mtu wangu, unadhani itakuwa sawa nchi za Afrika nazo waruhusu bangi ili kuongeza mapato ya kodi?
No comments:
Post a Comment