Nigeria wanafanya Uchaguzi Mkuu leo March 28 2015, moja ya vitu ambavyo vimekuwa vikisikika sana kutoka ndani ya nchi hiyo ni ishu ya mashambulizi ya kundi la Boko Haram, hivyo wengi wanafuatilia kwa ukaribu Uchaguzi huo kutokana na hali ya usalama kutokuwa nzuri.
Ripoti zimeonesha kuwa hali ni shwari na watu wanaendelea kupiga kura, kilichoripotiwa muda mfupi uliopita ni ishu ya Website ya Tume ya Uchaguzi kuvamiwa na wahalifu wa mitandaoni ambao wamehack na kuweka ujumbe ambao unaonya Tume hiyo kuhakikisha haifanyi udanganyifu wowote kwenye uchaguzi huo.
Ishu ya Website za Serikali ya Nchi hiyo kuvamiwa hii sio mara ya kwanza, iliwahi kuripotiwa pia story ya hackers kuvamia Website ya Bunge la Nchi hiyo.
Nigeria imekuwa kwenye Headlines kuhusishwa sana na ishu za hacking kwenye mitandao.
Jamaa waliovamia Website hiyo wanajiita ‘Jeshi la mtandaoni la Nigeria’ , Tume hiyo haijatoa taarifa yoyote mpaka sasa kama kuna athari yoyote itakayotokea kwenye Uchaguzi huo kutokana na uvamizi uliofanyika.
No comments:
Post a Comment