Ni
ajabu kusikia raisi wa nchi akitaka kupunguziwa muda wake wa kukaa
madarakani kwani wengi wao hufurahia maisha hayo na hutamani waendelee
kuongoza wananchi wao kwa maisha yao yote kusalia madarakani.
Hii imetokea huko Senegal baada ya rais wa nchi hiyo Macky Sall
kupendekeza kura ya maamuzi ili kupunguzwa kwa muhula wake wa kukaa
madarakani kwa miaka miwili ikiwa ni kinyume na ile ya viongozi wengine
wa Afrika ambao hutamani maisha yao yote kusalia madarakani.
Rais
huyo amesema alichaguliwa kwa miaka saba lakini mwakani mwezi Mei
anapendekeza kufanyika kwa kura ya maamuzi ili kupunguza kwa muda wake
ili kupisha wengine.
Sall alitoa ahadi hiyo ambayo ni baadhi ya ahadi zake alizotoa wakati wa kampeni za uchaguzi uliofanyika mwaka 2012.
No comments:
Post a Comment