Mpaka sasa ndani ya Marekani ni majimbo matatu ambayo wametoa ‘YES’ kuruhusu matumizi ya marijuana au bangi, Washington DC, Alaska na Colorado, lakini wataalamu wanasema kuna majimbo mengine ambayo yako njiani kuhalalisha matumizi hayo.
Barney Warf ni professor wa Chuo Kikuu cha Kansas, anasema ni ngumu kutabiri kuhusu jimbo lipi na lipi litahalalisha matumizi ya dawa hizo za kulevya, lakini majimbo haya matano aliyoyataja hapa kuna dalili zote bangi ikawa halali kwao, kutokana na kwamba kwa sasa bangi inatumika kama dawa nyingine za matibabu, hiyo kwake ni hatua ya kwanza kwenye kuelekea kuhalalisha matumizi kwa mtu yoyote.
Majimbo hayo ni California, Nevada, Vermont, Illinois na New York ambako Prof. Warfanasema muda si mrefu tutarajie kupitishwa kwa Sheria ya matumizi ya bangi kama kilevi cha kawaida ambacho kimehalalishwa.
No comments:
Post a Comment