Breaking News
recent

BARCELONA YAICHAKAZA REAL MADRID

Klabu ya Barcelona imeendelea kutikisa anga la soka baada ya hii leo kuichakaza Real Madrid kwa kuifunga mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Hispania uliopigwa Camp Nou usiku huu.
Barca ndiyo walioanza kutikisa nyavu kupitia kwa Jeremy Mathieu dakika ya 19, na Cristiano Ronaldo kusawazisha katika dakika ya 31.
Barca wamepata bao la pili kupitia kwa Luis Suarez dakika ya 57 na kuiwezesha Barcelona kuondoka na point point 3 muhimu.
Kwa matokeo hayo, Barcelona imezidi kujikita kileleni kwa kufikisha point 68 na kuiacha Real ikibaki nafasi ya Pili ikiwa na pointi 64 ikifuatiwa na Valencia yenye point 60.

Je, kwa mtazamo wako, unaipa asilimia ngapi Barcelona za kutwaa ubingwa wa Hispania msimu huu
Unknown

Unknown

No comments:

Powered by Blogger.