Rapa 50 cent amemtabiria ushindi bondia Floyd Mayweather katika pambano lake dhidi ya Manny Pacquiao litakalofanyika Mei 2 mwaka huu.
Pambano hilo linasubiriwa na mashabiki mbalimbali wa ngumi duniani kote ambapo rapa huyo amepanga kuweka dau la dola milioni 1.6 ambazo ni sawa na zaidi ya bilioni 2 za kibongo kwa kumtabiria ushindi ikiwa Mayweather ataibuka mshindi katika pambano ilo litakalofanyika katika mji wa Las Vegas.
Akizungumza katika kipindi cha ‘The Breakfast Club’ alisema alimfuata Mayweather katika onyesho la Chris Brown lililofanyika katika ukumbi wa Barclays Center mwezi uliopita kwa lengo la kuzungumza naye baada ya kimya cha muda mrefu na kumuahidi zawadi hiyo.
Cheki video hapo chini....
No comments:
Post a Comment