Kampuni ya Google inaanza kutengeneza magari yanayojiendesha yenyewe
badala ya kuboresha vyombo vya moto vilivyotengezwa na makampuni
mengine.
Magari hayo yatakuwa na vitufe vya kusimama na kujiendesha bila kuendeshwa na mtu,wala kuwa na usukani.
Picha za gari hilo zinaonyesha kuwa gari hilo ni kama mfano wa
magarimengine ya mjini yenye muonekano mzuri, yaliyobuniwa kuyafanya
yasitishe na kufanya watu wayakubali na kukubali teknolojia hiyo mpya.
Mgunduzi msaidizi wa magari hayo, Sergey Brin amebainisha mipango hiyo jijini California.
Lakini pamoja na hatua hiyo, watafiti wanachunguza juu ya uwezekano wa kutumika kwa teknolojia hiyo mpya.
No comments:
Post a Comment