Aliyekuwa kocha wa Manchester
United David Moyes anachunguzwa na polisi nchini Uingereza baada ya
kushtumiwa kuhusika katika mapigano katika baa moja ya mvinyo iliyoko
katika kitongoji cha Lancashire.
Maafisa wa polisi walifahamishwa saa nne usiku
saa za Uingereza kuhusu tukio ambalo kijana mmoja mteja katika baa ya
Emporium iliyoko Clitheroe alidai kapigwa na mtu ambaye ilibainika kuwa
ni kocha huyo aliyefutwa kazi wa Manchester United.Watu kadha walioshuhudia wamekuwa wakidai kuwa kijana huyo mwenye umri wa miaka 23 alimgoa kocha Moyes kutokana na matokeo duni ya Manchester United alipokuwa mkufunzi kwa miezi kumi na hivyo kumuudhi sana Moyes aliyemfokea na kumburuta.
Moyes alitimuliwa Old Trafford mapema mwezi huu yapata miezi 10 tangu achukue uskani kutoka kwa kocha mkongwe Sir Alex Fergusson aliyestaafu.
Alikuwa ametokea Everton ambayo alikuwa ameiongoza kwa zaidi ya miaka 10.
No comments:
Post a Comment