Matokeo ya awali yalionyesha kuwa chama hicho kimepata kura nyingi kiasi cha kuweza kutawala bila ushirikiano wowote na chama kingine.
Wafuasi wa upinzani wanasherehekeakatika makao makuu ya chama hicho.
Chama tawala cha Congress kimeshindwa baada ya kuwa mamlakani kwa miaka kumi
Kura ambazo zimehesabiwa kufikia sasa zinaonyesha kuwa muungano wa vyama unaoongozwa na chama BJP, chini ya Bwana Narendra Modi, utashinda kwa wingi wa kura.
Kiongozi wa BJP, Narendra Modi, anayetarajiwa kutangazwa kuwa Waziri Mkuu wa India.
Tume ya Uchaguzi ya India imesema kuwa matokeo ya awali yanathibitisha kuwa BJP kimeshinda viti 272, vinavyokiwezesha kutawala bila kushirikiana na chama kingine.
Zaidi ya watu milioni 500 walipiga kura ambayo ni asilimia 66 ya wote waliochaguliwa.
No comments:
Post a Comment