Ripota wa nguvu Simon Simalenga akiwa 104.4 Dodoma amekutana na Wanachuo
kwenye chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) ambapo kwenye bunge la bajeti
linaloendelea May 19 2014 Wabunge walipitisha bajeti ya wizara ya elimu
na mafunzo ya ufundi ambayo ni Bilioni 799.2
Ndani ya saa 24 toka kupitishwa kwa bajeti hiyo taarifa zinapatikana
kwamba kuna uwezekano wa kutokea maandamano ya Wanachuo wa chuo kikuu
cha Dodoma (UDOM) kuelekea bungeni kama hawatopata fedha zao za kujikimu
ambazo wamecheleweshewa kwenye collage yao ya Humanities.
Wanasema ‘hatujazungumza hivi sababu tumepanic, kikawaida chuoni
tunatakiwa kusaini boom kila baada ya siku 56 ambazo ziliisha 26 April
2014 na mpaka hatujapata taarifa yoyote toka wakati huo kwamba kuna
shida gani imetokea’
Mwajuma Ally ambae ni Mwanachuo wa UDOM pia amesema ‘niko mwaka wa pili,
tunashindwa kuelewa kwa nini hili tatizo limetokea mpaka sasa hivi
inaonekana sisi tunadharaulika manake hii ni mara ya pili inatokea
humanities lakini vyuo vingine wamepewa mikopo’
No comments:
Post a Comment