Anaitwa Davido Adeleke lakini kwenye muziki tunamjua
kama Davido ambae labda tatizo linalomkuta Davido ndilo lilelile kama
kwa Chris Brown na Justin Bieber yani kuwa na pesa nyingi na umaarufu
vyote katika umri mdogo.
Akiwa kwenye harakati zake za kwenda kwenye show Uingereza Davido
alifika airport na passport yake ya Marekani lakini maafisa wakamwambia
alete passport ya Nigeria kwa sababu passport hiyo ya Marekani haikuwa
na karatasi za visa ya kuingia Nigeria kwa hiyo utaratibu haujafuatwa.

Davido
alisisitiza kwamba anayo passport ya Nigeria lakini ameiacha nyumbani
hivyo hakuruhusiwa kusafiri hadi hiyo passport ya Nigeria ilivyoletwa
ndio akaruhusiwa kusafiri kisha baada ya hapo ali-tweet akiwatukana
maafisa wa airport kwa walichomfanyia.

Ofisi
ya maafisa wa uhamiaji wamesema tabia kama hiyo ya Davido Adeleke sio
sawa kabisa kwa sababu afisa huyo alifata utaratibu wa kazi ambao
umemsaidia Davido ambae huko mbele ya safari angeweza kurudishwa au
kuaibika zaidi kwani kwenye airport nyingine wako makini kwa hali ya juu
kwenye vitu kama hivyo na wasingemruhusu kuendelea na safari.
No comments:
Post a Comment