FUKO WA PENSHENI WA LAPF NI MFUKO WA HIFADHI YA JAMII NCHINI TANZANIA WENYE MAKAO MAKUU YAKE MJINI DODOMA.
MFUKO
WA LAPF UNAPENDA KUKANUSHA TAARIFA ZILIZOTOLEWA NA BAADHI YA VYOMBO VYA
HABARI KUWA LAPF ILITOA MSAADA KWA MBUNGE WA MBEYA MJINI MH. JOSEPH
MBILINYI NA MBUNGE WA IRINGA MJINI MH. PETER MSIGWA.
IELEWEKE KUWA INGAWA WAHESHIMIWA WABUNGE AU MTU AU
TAASISI YEYOYE HAWAZUILIWI KUOMBA MSAADA WA KIJAMII, MH. MBILINYI NA MH.
MSIGWA HAWAJAWAHI KUWASILISHA MAOMBI NA HAWAJAWAHI KUPEWA MSAADA WOWOTE
NA LAPF.
AIDHA LAPF INAKANUSHA HABARI ZILIZOTOLEWA KATIKA
GATEZI LA MTANZANIA LA TAREHE 26 MEI 2014 TOLEO NA. 7472 KUWA
WAHESHIMIWA WABUNGE NI WASUMBUFU NA KUMFANYA MKURUGENZI MKUU
ASIENDE BUNGENI.
LAPF INAKANUSHA PIA HABARI ILIYOTOLEWA KATIKA GAZETI
LA THE GUARDIAN LA TAREHE 27 MEI 2014 TOLEO NA. 6031. IELEWEKE KUWA
LAPF HAIJAWAHI KUMKOPESHA MH. FREEMAN MBOWE (kulia) KIASI CHA SHILINGI
BILIONI MOJA. MFUKO WA LAPF HAUNA UTARATIBU WA KUKOPESHA MTU MMOJA MMOJA
HIVYO HAKUNA MIKOPO YA AINA HIYO. LAPF HUTOA MIKOPO YA WANACHAMA WAKE
KUPITIA VYAMA VYA KUWEKA NA KUKOPA (SACCOS) NA MIKOPO YA NYUMBA KWA
WANACHAMA WANAOKARIBIA KUSTAAFU.
AIDHA, SI KWELI PIA KWAMBA LAPF HAISHIRIKI KATIKA
BAJETI YA OFISI YA WAZIRI MKUU KWANI MFUKO HUU UKO CHINI YA OFISI YA
WAZIRI MKUU TAMISEMI NA INASHIRIKI KATIKA VIKAO HIVYO.
LAPF
INAPENDA KUWAJULISHA UMMA WA WATANZANIA KUWA MFUKO HUTOA MISAADA YA
KIJAMII KWA KUZINGATIA MPANGO NA BAJETI ILIYOIDHINISHWA NA KWA
KUZINGATIA SERA YA MISAADA YA KIJAMII NA MAOMBI YANAYOWASILISHWA. PIA
HAKUNA TAASISI AU MTU BINAFSI INAYOPEWA FEDHA TASLIM ISIPOKUWA MFUKO
HUNUNUA VIFAA NA KUWASILISHA MOJA KWA MOJA KWA WAHUSIKA.
MFUKO WA PENSHENI WA LAPF UNAENDESHWA CHINI YA
SHERIA YA LAPF (THE LOCAL AUTHORITIES PENSIONS FUND ACT NO. 9 OF 2006).
SHERIA HII IMEFANYIWA MAREKEBISHO KUKIDHI MAHITAJI YA SHERIA YA
USIMAMIZI WA HIFADHI YA JAMII YA MWAKA 2008 (SSRA) NA KWA SASA LAPF
INAANDIKISHA WANACHAMA TOKA SEKTA ZOTE NCHINI NA JINA LA MFUKO
LILIREKEBISHWA NA SASA LINAJULIKANA KAMA MFUKO WA PENSHENI WA LAPF (LAPF
PENSIONS FUND).
SHUGHULI KUU ZA MFUKO NI PAMOJA NA KUANDIKISHA WANACHAMA, KUKUSANYA MICHANGO, UWEKEZAJI NA KULIPA MAFAO.
KWA
SASA LAPF INATOA MAFAO MBALI MBALI AMBAYO NI MAFAO YA UZEENI, MAFAO YA
MIRATHI, MAFAO YA KUUMIA KAZINI, MAFAO YA UZAZI, MAFAO YA KUJITOA,
MSAADA WA MAZISHI, MIKOPO YA NYUMBA, MIKOPO YA WANACHAMA KUPITIA SACCOS
NA IPO KATIKA HATUA ZA MWISHO ZA KUTOA MIKOPO YA ELIMU KWA WANACHAMA.
PAMOJA NA MAJUKUMU MAKUU YA MFUKO YALIYOTAJWA HAPO
JUU, MFUKO UNASHIRIKI PIA KATIKA KUISAIDIA JAMII NA HIVYO KUSAIDIA
KATIKA KUPUNGUZA UMASIKINI NA KUCHOCHEA MAENDELEO ( CORPORATE SOCIAL
RESPONSIBILITY).
MISAADA HII INA LENGO LA KUSAIDIA JAMII YOTE YA
WATANZANIA YENYE MAHITAJI MBALI MBALI NA KWA KUTAMBUA KUWA MISAADA HII
ITAWANUFAISHA SI WANACHAMA WA LAPF TUU BALI PIA WANANCHI WOTE.
LAPF IMEKUWA IKITOA MISAADA YA KIJAMII KATIKA SEKTA MBALI MBALI
KAMA VILE AFYA, ELIMU, VITUO VYA WATOTO YA YATIMA, TAASISI ZA WATU WENYE
MAHITAJI MAALUM, SEKTA YA MICHEZO NA KUSAIDIA MAAFA KWA KUTOA VIFAA
MBALI MBALI KAMA MASHUKA, VYANDARUA NA MADAWA, KATIKA ELIMU KUCHANGIA
UJENZI WA MADARASA, UNUNUZI WA MADAWATI NA VIFAA VYA MAABARA. KATIKA
VITUO VYA WATOTO YATIMA LAPF IMEKUWA IKITOA MISAADA YA VYAKULA, MAVAZI
NA VIFAA VYA SHULE. KADHALIKA KATIKA MICHEZO LAPF IMEKUWA IKICHANGIA
VIFAA VYA MICHEZO KAMA JEZI NA MIPIRA.
KWA MIAKA MITATU MFULULIZO MFUKO WA LAPF NDIO UMEKUWA MDHAMINI MKUU
WA MICHEZO YA JUMUIYA YA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU (TUSA) AMBAO NI
WANACHAMA WATARAJIWA WA MFUKO.
KATIKA MWAKA WA
FEDHA 2013/2014 MFUKO WA LAPF UMETOA MISAADA MBALI MBALI KAMA VILE VIFAA
VYA UJENZI CHUO CHA MADAKTARI BUGANDO NA CHUO KIKUU HURIA (OUT).
KADHALIKA LAPF IMEOTA VIFAA MBALI MBALI VYA SHULE KAMA VILE MADAWATI, TAA ZA SOLA NA MASHINE ZA FOTOKOPI.
KATIKA
SEKTA YA AFYA LAPF IMETOA MSAADA KWA HOSPITALI NA ZAHANATI MBALI MBALI
NCHINI KWA KUTOA VYANDARUA, MASHUKA, MADAWA, VIFAA VYA MAABARA, TAA ZA
SOLA PAMOJA NA KUCHANGIA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI.
KATIKA MICHEZO LAPF IMEENDELA KUWA MDHAMINI WA
MICHEZO YA JUMUIYA YA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU (TUSA) NA VIFAA VYA
MICHEZO KWA SHIRIKISHO LA SERIKALI ZA MITAA (SHIMISEMITA).
HII
NI BAADHI TU YA MISAADA AMBAYO LAPF IMETOA KWA MWAKA HUU KWA KUZINGATIA
MAOMBI MBALI MBALI YALIYOWASILISHWA PAMOJA NA BAJETI NA MPANGO WA MFUKO
ULIOIDHINISHWA. KWA MWAKA HUU WA FEDHA, MISAADA YOTE HADI SASA INA
JUMLA YA THAMANI YA SHILINGI MILIONI MIA MOJA NA ISHIRINI. AIDHA,
KUTOKANA NA UFINYU WA BAJETI YA MFUKO, SEHEMU KUBWA YA MISAADA HII NI
KATI YA SHILINGI LAKI TANO HADI MILIONI TATU. MISAADA HII HUTOLEWA MOJA
KWA MOJA KWA WALENGWA NA PIA SI FEDHA TASLIMU, BALI VIFAA HUSIKA.
No comments:
Post a Comment