Milipuko na risasi zimesikika katika mji mkuu wa
Somalia Mogadishu huku majengo ya bunge la Somalia yakishambuliwa,
wabunge wakiwa ndani kwa mkutano.
Haijajulikana waliofanya mashambulizi hayo ambayo bado yanaendelea.Wabunge wawili wameuawa chini ya mwezi mmoja |
Bunge la kwanza rasmi la Somalia lilianza kufanya kazi miaka miwili iliyopita tangu Somalia kutumbukia katika vita mwaka 1992.
Serikali ya Somalia imekuwa ikiendesha vita dhidi ya kundi la kiisilamu la al-Shabab ambalo lilitimuliwa kutoka mjini Mogadishu mwaka 2011.
Bunge hilo, ambalo huendesha vikao vyake mjini Mogadishu limewahi kushambuliwa ikiwemo mwaka 2009 na 2010.
Mwezi jana Mbunge mmoja aliuawa kwa kulipuliwa huku mwingine akipigwa risasi na kuuawa katika mashambulizi mawili tofauti.
Wanajeshi 22,000 walio chini ya muungano wa Afrika wanasaidia vikosi vya Somalia kupambana na Al Shabaab.
Ingawa kundi hilo limepoteza udhibiti mkubwa wa miji kadhaa nchini Somalia, bado linadhibiti maeneo mengi ya vijijini.
No comments:
Post a Comment