RB namba WH/RB/6335/2014-SHAMBULIO LA KUDHURU MWILIkwenye
Kituo cha Polisi cha Wazo Hill, Tegeta jijini Dar, imemtia mbaroni
mtangazaji maarufu Bongo aitwaye Hanifa Hamidu ‘Lady Hanifa’ na mwenzake
aliyetajwa kwa jina moja la Aneth kwa madai ya kutaka kumuua mhudumu wa
baa aliyetambulika kwa jina la Aika Andrew (32).
Mtangazaji maarufu Bongo aitwaye Hanifa Hamidu anayetuhumiwa kumshambuli mhudumu wa baa.
Uchunguzi
wa gazeti hili ulibaini kwamba sakata hilo la kusikitisha lilijiri wiki
iliyopita kwenye baa maarufu ya Shayo iliyopo Tegeta, Dar.
Maelezo yaliyoandikishwa na Aika polisi yalidai kwamba Lady Hanifa alifika kwenye baa hiyo ambayo ndani yake anamiliki jiko la chakula na kuelezwa kwamba, siku moja kabla ya tukio hilo alikuwa na deni na alipofika tu, Aika alimkumbushia ndipo balaa lilipoanza.

Mhudumu wa baa anayetambulika kwa jina la Aika Andrew (32) aliyenusurika kuuawa na mtangazaji maarufu Bongo, 'Lady Hanifa' .
Kwa
mujibu wa mashuhuda, katika tukio hilo lililojiri mishale ya saa 11:00
jioni, Hanifa alipofika aliingia moja kwa moja jikoni kuangalia biashara
yake kisha akarudi kukaa sehemu ya baa.
Ilisemekana kwamba Aika alimfuata na kumwambia kuwa jana yake alikuwa akidaiwa bia moja tu ya baridi aliyokuwa amekopa, kitendo kilichompandisha hasira na kuona kama amefedheheshwa kudaiwa mbele za watu.

Majeraha ya moto shingoni mwa Aika Andrew.
Ilidaiwa
kwamba alimwita mfanyakazi wake, Aneth ili ampatie fedha aliyokuwa
akidai Aika lakini muda huohuo Lady Hanifa akaanza kudai chenji yake
kwa mabavu.
Ilidaiwa kwamba kulitokea majibizano makubwa ndipo mtangazaji huyo akaanza kumshambulia Aika huku akipewa sapoti na Aneth.
Ilidaiwa kwamba kulitokea majibizano makubwa ndipo mtangazaji huyo akaanza kumshambulia Aika huku akipewa sapoti na Aneth.
Wasamaria wema wakimpeleka Hospitali ya Mwananyamala, Aika Andrew.
Iliendelea
kudaiwa kwamba katika purukushani hizo, Aneth aliyekuwa ameshika kisu
alimchoma nacho Aika tumboni, kichwani, mikononi huku Lady Hanifa
akimuunguza shingoni kwa kutumia upawa wa chipsi uliokuwa na mafuta ya
moto kisha wakakimbia.
Habari
zilieleza kwamba baada ya hapo Hanifa na Aneth walikimbilia Kituo cha
Wazo Hill kutoa taarifa lakini muda mfupi wasamaria wema walifika katika
kituo hicho wakiwa na Aika aliyekuwa ametapakaa damu mwili mzima.
Polisi waliwashikilia Lady Hanifa na Aneth na Aika akakimbizwa Hospitali ya Mwananyamala.
SOURCE: GPL
Polisi waliwashikilia Lady Hanifa na Aneth na Aika akakimbizwa Hospitali ya Mwananyamala.
SOURCE: GPL
No comments:
Post a Comment