Breaking News
recent

EPL: ROONEY ATOLEWA KWA KADI NYEKUNDU, HAYA NDIYO MATOKEO YA MANUTD VS WESTHAM

article-2771941-21B6773E00000578-530_964x386 Ligi kuu ya Uingereza imeendelea tena leo huku klabu ya Manchester United ikijitupa uwanjani kucheza dhidi ya West Ham katika kuusaka ushindi wa pili kwenye ligi hiyo tangu ilipoanza.
Katika mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa Old Trafford, nahodha wa klabu ya Manchester United Wayne Rooney alifanya makosa ya kizembe yaliyomsababishia kadi nyekundu ya moja moja baada ya kumkata mtama Stewart Downing na hivyo atakosa mechi 3 zijazo za premier league.
Pamoja na Rooney kuwaangusha wachezaji wenzie kwa kadi nyekundu ya kujitakia, lakini Manchester ilifanikiwa kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya vijana wa Sam Alladyce.
Rooney alianza kuifungia United goli dakika za mwanzo tu za mchezo na dakika kadhaa baadae Robin van Persie akaiandikia timu yake goli la pili.
West Ham walitulia na kujipanga vizuri na kufanikiwa kufunga goli lao moja kupitia Sakho baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Man United.
Man United walicheza kwa zaidi ya dakika 40 wakiwa pungufu baada ya Rooney kupewa kadi nyekundu.
TIMU ZILIPANGWA HIVI….
Manchester United (4-1-2-1-2): De Gea 6; Rafael 6, McNair 7, Rojo 6, Shaw 6; Blind 7; Herrera 7 (Valencia 74 6), Di Maria 6 (Thorpe 90 6); Rooney 4; Van Persie 7, Falcao 6 (Fletcher 65 6).
Sent off: Rooney.
Booked: Herrera.
West Ham (4-3-1-2): Adrian 5; Demel 6 (Jenkinson 65 6), Tomkins 6, Reid 5, Cresswell 6; Song 5, Poyet 6, Amalfitano 6 (Cole 61 6); Downing 6: Sakho 7, E Valencia 6.
Booked: Song, Sakho.
Referee: L Mason.
Man of the match: Blind.
Unknown

Unknown

No comments:

Powered by Blogger.