Kwa muda mrefu kumekuwa na mjadala mkubwa ikiwa
mjasiriamali anazaliwa au anatengenezwa. Kwa kuangalia tabia za
wajasiriamali na tabia za binadamu kwa ujumla, wajasiriamali wana tabia
za kipekee. Wajasiriamali wanafikiri tofauti na wanatenda tofauti na
watu wengine kwenye jamii.
Tabia za kipekee
zinazooneshwa na wajasiriamali kuna ambao wamezaliwa nazo na kuna ambao
wamezipata kutoka kwenye mazingira na shughuli wanazofanya.
Hapa
nitaelezea tabia thelathini(30) ambazo ni dalili tosha kwamba wewe ni
mjasiriamali. Kama huna tabia hizi unaweza ukaanza kujifunza taratibu na
baadae ukawa na tabia za kijasiriamali. Kumbuka tofauti kubwa ya
mjasiriamali ni jinsi anavyofikiri na kuchukua hatua tofauti na watu
wengine. Kwa mfano wakati mwajiriwa anaweza kukubaliana na shida
anazopata kwenye ajira yake na kuona hakuna anachoweza kufanya,
mjasiriamali anafikiria uwezo wa tofauti alionao na jinsi anavyoweza
kwenda kuutumia nje ya ajira na akafanikiwa. Baada ya hapo anaweza
kuacha kazi na kwenda kufanya lile litakalomridhisha. Kwa kuwa na
mtizamo chanya na utayari wa kuchukua hatua kunawafanya wajasiriamali
kupata mafanikio makubwa.
Kama
unatabia hizi 30, ni dalili tosha kwamba wewe ni mjasiriamali,
unatakiwa kuchukua hatua mara moja ili kufikia mafanikio makubwa;
1.
Hukubaliani na mfumo. Mara nyingi umekuwa ukihoji kwa nini kitu fulani
kifanyike na umekuwa ukijitahidi kutafuta njia bora zaidi ya kufanya
kazi fulani pale unapokuwa umeajiriwa. Hufanyi kitu bila ya kuhoji
umuhimu wake na kufikiri njia ya kuboresha.
2.
Unaonekana kama mfanyakazi mkorofi. Wakati mwingine umeshafukuzwa kazi
mara kadhaa kutokana na tabia yako ya kuhoji na kutaka kuboresha
utendaji kazi. Au umeshaacha kazi au kupanga kufanya hivyo kutokana na
kutoridhishwa na kazi hiyo.
3. Una hamasa
kubwa ya kutekeleza majukumu yako. Husubiri upangiwe cha kufanya, unajua
majukumu yako na unayafanya kwa ubora wa hali ya juu.
4. Ukiambiwa hapana huridhiki, hapana sio jibu kwako unaendelea kutafuta njia nyingine mpaka upate NDIYO.
5.
Unajiamini na unaamini una uwezo mkubwa wa kufanya mambo makubwa. Una
uhakika hata kitokee kitu gani bado unauwezo wa kusimama na kuleta
tofauti.
6. Ni mtu wa watu, unaweza
kuchangamana na watu wa aina zote. Huna ubaguzi wa aina gani ya watu
unaweza kukaa nao, popote unapokutana na watu unaweza kuanzisha
mazungumzo na mkaenda vizuri.
7. Huogopi sana juu ya usalama wa ajira kwani unaamini hata bila ya ajira bado unaweza kuendesha maisha yako.
8.
Mara kadhaa umekuwa ukigomea mamlaka. Umekuwa ukikataa maelekezo
yanayotolewa na mamlaka kama hayaendani na misimamo yako ya ufanyaji
kazi bora. Hii imekupelekea kuonekana ni mfanyakazi mkorofi na hata
kufukuzwa.
9. Siku za mapumziko kama
sikukuu au mwisho wa wiki ndio siku bora kwako kufanya kazi zako
binafsi, huendekezi kupoteza muda kwa kupumzika au kustarehe.
10. Umewahi kuuza vitu vidogo vidogo ulipokuwa mtoto. Pia umewahi kufuga kuku, sungura na hata njiwa enzi za utoto wako.
Unknown
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment