Cristiano
Ronaldo jana alicheza mechi yake ya 100 ya ligi ya mabingwa wa ulaya
wakati Real Madrid walipoifunga Borussia Dortmund 3-0.
Katika mechi hiyo Ronaldo alifunga goli la 3 la mchezo huo baada ya Bale na Isco kufunga la kwanza na lapili.Kwa goli hilo moja sasa amefikisha jumla ya mabao 14 katika msimu huu wa ligi ya mabingwa wa ulaya, hivyo amemfikia Messi aliyeweka rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi katika msimu mmoja wa ligi ya mabingwa wa ulaya msimu wa 2011/12 – magoli 14.
No comments:
Post a Comment