Breaking News
recent

WATOTO WA MJINI NOMAAAAA, CHEKI ALICHOMFANYA HUYU RAIA WA KIZUNGU

Raia mmoja wa nchini Finland amejikuta katika wakati mgumu sana baada ya kushindwa kufanya lolote kazini alipoajiriwa baada ya kutaka kuwa katika mahusiano na mwanadada huyu wa chuo kikuu cha Dar es salaam ambaye alimteka akili kiasi cha kumfanya Mzungu huyo kuwa anashinda chuoni kutwa nzima kubembeleza akubaliwe jambo lililomsababishia aache kuhudhuria kazini kwa muda wa miezi mine mfululizo kutokana na kupagawishwa na uzuri wa mwanadada huyu ambao umemfanya awe gumzo chuo kizima.

Mzungu huyo  ambaye ni muajiriwa wa kampuni moja ya simu za mkononi (Jina limehifadhiwa) hapa jijini alikuja Tanzania mwaka jana kwa dhumuni la kufanya kazi kwa mkataba amejitia matatizoni baada ya kumtaka kimapenzi mrembo huyu ambaye alikutananae kwa mara ya kwanza katika coffe bar moja iliyopo Mlimani city na kwakushindwa kuzuia hisia zake alijikuta akiomba mawasiliano ya mrembo huyu jambo ambalo ndio hasa limemsababishia matatizo kutokana na ukweli kwamba Mzungu huyo amekuwa akimbembeleza sana mrembo huyu bila mafanikio  kiasi cha kumfanya aweanashinda Chuoni kwa huyu dada huyu Mlimani main campas. 

Utoro sugu wa Mzungu huyo umemuweka katika wakati mgumu kwani amepewa barua mbili za onyo mpaka sasa na amebakiza barua ya mwisho aachishwe kazi jambo ambalo mwenyewe anasema kuwa yuko katika wakati mgumu sana kwani hayuko tayari kumkosa dada huyo licha ya ukweli kwamba nchini kwao ameacha mke na watoto. 

Nilipomfanyia mahojiano dada huyo alidai hawezi kuwa na mtu ambaye hana malengo nae ya muda mrefu kwani uwepo wake hapa nchini ni wa muda mfupi tu hivyo yeye hayuko tayari kuwa kama chombo cha starehe kwa kila mpita njia. Licha ya kumpongeza dada huyo nilitaka nifahamu kama ameshamwambia ukweli Mzungu huyo ambapo dada alieleza kuwa ukweli ameshamwambia lakini jamaa huyo amekuwa king’ang’anizi kiasi cha kumnyima mpaka muda wa kujisomea jambo linalomfanya akate shauri la kwenda kumripoti katika kituo cha polisi kilichopo chuoni hapo endapo kesho siku ya kesho atathubutu kumfata tena.
Unknown

Unknown

No comments:

Powered by Blogger.