Akizungumza hapo jana na Rais Francois Hollande wa Ufaransa katika ikulu ya Elizer huko Paris, Rais Catherine Samba Panza wa Jamhuri ya Afrika ya Kati amesema kuwa wamesikia ahadi na maneno mengi kutoka kwa washirika wa Magharibi, hata hivyo nchi hizo zimeshindwa kuitimizia nchi yake ahadi ilizotoa.
Rais Panza amesisitiza pia kwamba, Jamhuri ya Afrika ya Kati inaiomba jamii ya kimataifa iharakishe mchakato wa kutekeleza ahadi hizo kwa kuzingatia hali mbaya ya mambo iliyoko nchini humo.
Katika mazungumzo hayo, Rais Hollande pia amesisitiza juu ya kuisaidia serikali ya mpito ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na kutimiza ahadi ilizotoa katika sekta ya usafirishaji, afya na misaada ya kilojistiki kwa nchi hiyo.
Hii ni katika hali ambayo zaidi ya watu elfu mbili wameuliwa huko Jamhuri ya Afrika ya Kati na wengine zaidi ya theluthi moja ya jamii ya watu milioni nne na laki sita wa nchi hiyo wamelazimika kuyahama makazi yao kutokana na kuendelea machafuko na mauaji nchini humo tangu mwezi Disemba mwaka jana hadi sasa.
KUSHOTO
RAIS WA JAMHURI YA AFRIKA YA
KATI BI. SAMBA
PANZA.
No comments:
Post a Comment