MWILI WA MAREHEM NGWEA KUFIKA SIKU YA JUMAPILI BADALA YA JUMAMOSI NA KUAGWA JUMATATU
Kamati ya mipango ya mazishi ya marehem Ngwea
wametoa taarifa mpya kwamba mwili wa ndugu yetu Albert Mangwea utafika siku ya
juma pili ya tarehe 2 / 6 saa nane mchana na sio siku ya jumamosi kama
ilivyotaarifiwa hapo awali.
sababu za mwili wa Albert Mangwea kushindwa
kufika jumamosi kama ilivyopangwa ni kutokana na watanzania waishio Africa
Kusini, kuomba na wao kutoa heshima za mwisho
kwa maana hiyo basi taratibu zote za kuaga mwili
wa marehemu Albert Mangwea, kwa wakazi wa Dar es salaam na maeneo ya jirani
zitafanyika siku ya jumatatuya tarehe 3 / 6 kuanzia saa mbili ya asubuhi mpaka
saa sita mchana, ambapo baada ya hapo, safari rasmi ya kuelekea Mororgoro
itaanza kwa ajili ya mazishi itaanza.
kamati inaomba radhi kwa usumbufu wowote
uliojitokeza
No comments:
Post a Comment