Breaking News
recent
                                           MATOKEO KIDATO CHA IV BALAA
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa
HATIMAYE, matokeo ya kidato cha nne kwa wanafunzi waliohitimu mwaka jana, yametangazwa upya. Matokeo hayo yalitangazwa jana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Alisema kwamba, pamoja na Serikali kutumia mfumo mpya wa uchakataji uitwao fixed grade range ambao ilisema umeboreshwa kisha kufanyiwa utafiti na wataalam wa Wizara ya Elimu na Mafunzo, bado matokeo hayo ni mabaya kwani waliofaulu wameongezeka kwa asilimia tisa ikilinganishwa na matokeo ya awali yaliyotangazwa Februari 8, mwaka huu.
Kutokana na hali hiyo, wanafunzi watakaojiunga na kidato cha tano pamoja na vyuo, watatangazwa mwezi ujao na Julai watajiunga na shule na vyuo watakavyokuwa wamepangiwa. Kwa mujibu wa Dk. Kawambwa, kutangazwa kwa matokeo hayo, kumeyafuta rasmi matokeo ya awali.

Katika maelezo yake, Dk. Kawambwa alisema wanafunzi waliopata daraja la kwanza ni 3,242 sawa na asilimia 0.88, daraja la pili ni 10, 355 sawa na asilimia 2.8, daraja la tatu ni 21, 752 sawa na asilimia 5.87 na kwamba ufaulu wa daraja la kwanza hadi la tatu ni sawa na asilimia 9.55.

Waliopata daraja la nne alisema ni 124,260, sawa na asilimia 33.54 na waliopata daraja sifuri ni 210,846 sawa na asilimia 56.92.

Kutokana na matokeo hayo, alisema waliopata daraja la kwanza hadi la nne ni 159, 747 ambao ni sawa na asilimia 43.08.

“Kwa ujumla, baada ya marekebisho, hakuna wanafunzi walioshuka daraja kwani waliofaulu awali walikuwa ni asilimia 34.05 na sasa ufaulu umeongezeka na kufikia asilimia 43.08.

“Hata hivyo, ufaulu huo bado upo chini kwa kuwa mwaka 2011 waliofaulu walikuwa ni asilimia 53.
 MIKOA ILIYOFELIDk. Kawambwa aliitaja mikoa iliyoshika mkia kuwa ni Mtwara, Lindi, Pwani na Tanga.
SHULE ZILIZOFAULU
Dk. Kawambwa alizitaja shule zilizofaulu katika kumi bora kuwa ni St. Francis Girls (Mbeya), Marian Boys (Pwani), Feza Boys (Dar), Marian Girl’s (Pwani), Canossa (Dar), Feza Girl’s (Dar), Rosmini (Tanga), Anwarite Girls (Kilimanjaro), St Mary’s Mazinde Juu (Tanga) na Jude Moshono (Arusha).

Shule zilizoshika mkia ambazo nyingi ni za Serikali ni pamoja na Mibuyuni (Lindi), Mamndimkongo (Pwani), Chitekete (Mtwara), Kikale (Pwani), Zirai (Tanga), Matanda (Lindi), Kwamndolwa (Tanga), Chuno (Mtwara), Mbembaleo (Mtwara) na Maendeleo (Dar es Salaam).

Naye Naibu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Charles Msonde, alisema matokeo hayo yalipitiwa kitaalam na hakuna mwanafunzi aliyeshuka daraja kutoka katika matokeo ya awali japokuwa waliokuwa wamefeli awali, baadhi wamefanikiwa kupanda madaraja

MATOKEO YA AWALIAkitangaza matokeo ya awali, Februari mwaka huu, Dk. Kawambwa alisema jumla ya watahiniwa walikuwa ni 126, 847 kati ya 397,136 waliofanya mtihani huo, walifaulu na watahiniwa 270,289 hawakufaulu.

Alisema wanafunzi 240,903 walipata daraja sifuri wakiwamo wasichana 120,664 na wavulana 120,239.

Waliopata daraja la kwanza ni 1,641, daraja la pili ni 6,453, daraja la tatu ni 15,426 na daraja la kwanza hadi la tatu ni 23,520 wakati daraja la nne ni watahiniwa 103,327.

Dk. Kawambwa alizitaja shule 20 zilizofanya vizuri kuwa ni St. Francis Girls (Mbeya), Marian Boys (Pwani), Feza Boys (Dar), Marian Girls (Pwani), Rosmini (Tanga), Canossa (Dar),Jude Moshono (Arusha), St. Mary’s Mazide Juu (Tanga), Anwarite Girls (Kilimanjaro), Kifungilo Girls (Tanga)

Nyingine ni Feza Girls (Dar), Kandoto Sayansi Girls (Kilimanjaro), Don Bosco Seminary (Iringa), St. Joseph Millenium (Dar), St. Joseph Iterambogo (Kigoma), St. James Seminary (Kilimanjaro), Mzumbe (Morogoro), Kibaha Sekondari (Kibaha), Nyegezi (Mwanza) na Tengeru Boys (Arusha).

Shule 10 za mwisho ni Mibuyuni (Lindi), Ndame (Unguja), Mamndimkongo (Pwani), Chitekete (Mtwara), Maendeleo (Dar), Kwamndolwa (Tanga), Ungulu (Morogoro), Kikale (Pwani), Nkumba (Tanga) na Tongoni (Tanga).
Unknown

Unknown

No comments:

Powered by Blogger.