Breaking News
recent
UNAAMBIWA MANCHESTER UNITED IMEKARIBIA KUMSAJILI HUYU MKALI


imageNahodha wa kikosi cha timu ya taifa ya Hispania kwa vijana wenye umri chini ya miaka 21 Thiaggo Alcantarra yuko mbioni kujiunga na klabu ya Manchester United ambayo iko tayari kutoa paundi milioni 15 kwa ajili yake.
Thiago Alcantarra ambaye Barcelona iliweka kipengele kwenye mkataba wake kinachoitaka timu yoyote inayotaka kumsajili kulipa paundi milioni 90, anaweza kuuzwa kwa bei ya chini zaidi ya hapo baada ya kucheza mechi zisizozidi 15 msimu uliopita na Thiago mwenyewe anataka kwenda mahali ambako atakuwa na uhakika wa kucheza kwenye kikosi cha kwanza.
Barcelona inamtazama Thiago kama mrithi wa nafasi ya Xavi kwenye kikosi chake lakini wanataka mchezaji huyo avumilie kukaa benchi kwa muda zaidi wakati mkongwe huyo (Xavi) akiwa bado kwenye kiwango chake ambapo pia kocha wa Man United David Moyes amekuwa akimfuatilia Thiago kwa muda mrefu tangu akiwa Everton japo alikuwa akifahamu kuwa Everton haina uwezo wa kumnunua.
Mchezaji wa Barcelona Gerard Pique kwa upande mwingine amesikika akimshawishi Tiago kubaki Barcelona kwa kuwa ni sehemu ya Maisha yake na hakuna mahali anakoweza kupata furaha zaidi ya Barca, anasema anapaswa kuwaangalia kina Xavi pamoja na Andres Iniesta ambao walikuwa wavumilivu kungojea wakati wao na wakafikia mafanikio makubwa wakiwa na Barca na kwenye soka la kimataifa .
Unknown

Unknown

No comments:

Powered by Blogger.