Kuna watu ambao sio watumiaji wazuri wa
mitandao ya kijamii, wapo ambao wanaandika lugha ambayo sio nzuri, hii
inatokana na kutokuwepo utaratibu rasmi wa kujisajili kwa kutumia majina
sahihi.
Tumeshuhudia account nyingi mitandaoni
ambazo wanaoziendesha sio wahusika wenyewe, ziko zenye majina ya mastaa,
viongozi, lakini ukweli ni kwamba wanaoziendesha sio wenye majina hayo.
China ni moja ya nchi ambazo
zimefanikiwa kuzuia vitu vingi mitandaoni , safari hii utaratibu ambao
wameutangaza utaratibu mpya, kama unafungua accountt yako kwenye mtandao
wowote wa kijamii ikiwemo Weibo ambao uko kama Twitter, Blogs na mingineyo ni lazima ufungue kwa jina lako kamili, hakuna a.k.a hakuna nickname inayotakiwa.
Kama ikitokea ukafanya usajili kwa jina
fake account yako itazuiwa na hutoweza kuitumia, wamefanikiwa kuzuia
mengi na hii wanaamini watazuia ‘utapeli’ wa majina ya uongo ambayo yako
mitandaoni.
Unaambiwa hata ukitaka kucomment chochote kilichoandikwa mtandaoni lazima ujisajili mtu wangu, hii kama ikija Bongo unaonaje labda?
No comments:
Post a Comment