Breaking News
recent

REAL MADRID, MANCHESTER CITY, LIVERPOOL, ARSENAL ZABANWA VILIVYO, CHELSEA AZIDI KUKWEA POINT 7 JUU

(null)
Baada ya kushindwa kupata ushindi katika mechi 5 mfululizo dhidi ya wapinzani wao wa jadi kabisa – Real Madrid leo walivuka kutoka upande mmoja wa mji wa Madrid na kwenda mpaka katika dimba la Vicente Carlderon pembezoni mwa jiji la Madrid kucheza dhidi ya Atletico Madrid.
Mchezo huo uliokuwa unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa timu zote mbili umemealizika kwa Madrid kupata kipigo kizito kabisa katika kipindi cha miezi 12 iliyopita – kwa kufungwa 4-0.
Magoli ya Atletico Madrid yalifungwa na Tiago, dakika ta 14, Ñíguez dakika ya 18, Griezmann akaongeza 67 kabla ya Mandzukic kuongeza dakika za mwisho za mchezo huo.
Hii ni mechi ya sita mfululizo Madrid wanashindwa kupata matokeo chanya dhidi ya wapinzani wao.
Tukielekea katika premium ligi
256D4BC100000578-0-image-a-89_1423318735904

Tottenham Hotspurs wamefanikiwa kuwafunga Arsenal katika mchezo wa ligi kuu ya England uliopigwa hii leo (Jumamosi) kwenye uwanja wa White Hart Lane ukiwa mchezo wa kwanza wa ligi hiyo kwa ratiba ya jumamosi .
Arsenal ndio walianza mchezo huo kwa kasi zaidi wakipata bao la kwanza kupitia kwa kiungo mshambuliaji Mesut Ozil ambaye alifunga kwenye dakika ya 11  .
Spurs walisawazisha  bao hilo kupitia kwa mshambuliaji chipukizi Harry Kane ambaye alifunga kwenye dakika ya  56 ya mchezo zikiwa zimepita dakika 9 tangu kuanza kwanza kipindi cha pili . Kane aliwahakikishia Tottenham pointi zote tatu kwenye dakika ya 86 kwa kufunga bao la pili bao ambalo limewapaisha Spurs mpaka kwenye nafasi ya 4 kwenye msimamo wa ligi kuu ya England.
Kane hadi sasa amefunga mabao 12 kwenye ligi hiyo ambapo anashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa wafungaji akiwa nyuma ya Diego Costa , Sergio Aguerro  na Charlie Austin .
(null)
Baada ya kucheza dakika takribani 660 kufunga goli katika ligi kuu ya England, hatimaye leo hii Aston Villa wameweza kuona nyavu katika mchezo wao dhidi ya viongozi wa ligi hiyo Chelsea.
Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Villa Park jioni ya leo, umemalizika kwa Villa kumaliza ukame wa magoli lakini haikutosha kuwapa matokeo chanya dhidi ya Chelsea.
Magoli mawili ya Eden Hazard na Branslav Ivanovic yalitosha kuipa Chelsea pointi 3 muhimu dhidi ya Villa.
Katika upande mwingine Southampton wamerudi nafasi ya 3 kwenye msimamo baada ya kuifunga QPR 1-0, huku Man City wakikabwa koo na Hull City kwa kutoka sare ya 1-1. Liverpool nae yupo katoka sare ya bila kufungana dhidi ya Everton
Unknown

Unknown

No comments:

Powered by Blogger.