Umri wa Jose Mujica ni miaka 78 ambapo May 20 mwaka huu anatimiza miaka 79
1.
Yani nguo zake zinafuliwa kawaida na kuanikwa nje tu, pia maji anayotumia ni ya
kisima ambacho kina magugu mengi.
2.
Analindwa na Polisi wawili na mbwa na aliikataa kukaa kwenye nyumba ya serikali
aliyopewa na badala yake kaenda kuishi kwenye nyumba ya mke wake huko mashambani
ambako kuna mazingira ya kimasikini sana ikiwemo barabara mbovu nje kidogo ya
mji wa Montevideo.
3. Rais na mkewe hufanya kazi ya kuotesha maua wao wenyewe
yakiwa ni maisha ya kipekee kusikia ni ya Rais wa nchi.
4. Mujica anatoa
asilimia tisini 90% ya mshahara wake wa kila mwezi kusaidia watu masikini huku
akisema ‘naweza kuonekana kama mzee wa jadi lakini maisha haya nimeyachagua
mwenyewe, naweza kuishi vizuri na kile nilichonacho.
5.
Rais huyu kwa mwezi matumizi yake hayazidi shilingi milioni moja laki nne za
Kitanzania ambapo kwenye kuorodhesha kiwango cha kipato cha kila kiongozi kwa
mwaka na mali binafsi ikiwa ni lazima nchini humo kwa viongozi mbalimbali wa
serikali mwaka 2010, alikutwa na kiasi cha dollar $ 1,800 tu kiasi ambacho
hakizidi shilingi milioni tatu za kitanzania.
6.
Gari anayotumia ndio hiyo picha ya kwanza hapo juu ambayo ni ya mwaka 1987 aina
ya Volkswagen Beetle.
7. Mujica aliwahi kupigwa risasi mara sita na alitumikia kifungo miaka 14 jela ambapo muda wake mwingi kizuizini alikua katika mazingira magumu na kutengwa, mpaka alipoachiliwa huru mwaka 1985 wakati Uruguay ilivyorudi kwenye demokrasia.
8.
Akiwa jela Mujica anasema hali ile ilimbadilishia mtazamo wake juu ya maisha na
anakwambia ‘mimi naitwa rais maskini
lakini mimi wala sihisi umaskini wowote, watu masikini ni
wale ambao kazi yao ni kuishi maisha ya gharama ambayo inawasababisha kufanya
kazi sana ili waendelee na maisha ya gahrama na kupata zaidi’
- Mujica aliwalaumu viongozi wengi wa dunia ya kuwa na “upofu wa kutaka kukua na matumizi, kiasi kwamba isipokua hivyo itakuwa mwisho wa dunia.
Nyumbani kwake
Nyumbani kwake.
No comments:
Post a Comment