ALICHOSEMA MDOGO WAKE TONI KROOS KUHUSU KAKA YAKE KUJIUNGA NA MANCHESTER UNITED
Wakati tetesi za usajili wa Toni Kroos kutakiwa na Manchester United zikizdi kupamba moto, Felix Kroos, mwanasoka anayekipiga katika klabu ya Werder Bremen, amesema kwamba ndugu yake, ambaye ni kiungo wa Bayern Munich, anaweza kujiunga na Manchester United msimu ujao.
Toni Kroos ambaye mkataba wake na Bayern Munich unaisha mwishoni mwa msimu ujao, mazungumzo yake ya mkataba mpya na Bayern yamekwama na Manchester United wamekuwa wakihusishwa na kumsajili tangu mapema January wakati kocha David Moyes alipoonekana na wakala wa mchezaji.
Sasa mdogo wa mchezaji huyo, Felix Kroos ameiambia Sky Germany: “Tumeshaongea kuhusu hilo jambo la Toni kuhamia Manchester United].
“Manchester imekuwa timu ya ndoto zangu tangu nilipokuwa mtoto. Japokuwa mie sijampa ushauri wowote.
“Atachukua maamuzi mazuri kwa ajili yake.”
No comments:
Post a Comment