Baada ya kuonewa kwa muda mrefu na majiraji zao katika ligi kuu ya England, hatimaye leo jiji la Manchester limepakwa rangi nyekundu baada ya kuisha kwa mchezo kati ya Manchester United vs Man City.
Mchezo huo uliomalizika hivi punde katika dimba la Old Trafford umeshuhudia Man United wakirudisha utawala wao dhidi ya City kwa kuwapa kipigo cha magoli 4-2.
Magoli ya City yalifungwa na Sergio Aguero yote mawili, na huku United yao yalifungwa na Ashley Young, Juan Mata, Maroune Fellaini na Chris Smalling.
Chelsea wao walicheza mchana na QPR na kushinda 1-0, goli la Cesc Fabregas.
Manchester United watasafiri kuelekea Stamford Bridge wikiendi ijayo kucheza na Chelsea.
MSIMAMO WA LIGI ULIVYO
VIDEO YA MAGOLI YOTE YA MANCHESTER DERBY...
No comments:
Post a Comment