Watoa huduma za uokoaji huko mji mkuu wa Nepal Kathmandu, wamefanikiwa kumuokoa kijana mmoja mwenye umri wa miaka 15 aliyepatikana hai baada ya funikwa na vifusi vya jengo alilokuwemo wakati wa tetemeko la ardhi kukumba taifa hilo siku tano zilizopita.
Licha ya kuwa chini ya maporomoko hayo kwa siku hizo tano isaidiwa na mwanya uliokuwa ukipenyeza hewa iliyomwezesha kupumua japo kwa shida.
Makundi ya watu walimshangilia alipotolewa huku akionekana akijitahidi kufungua macho yake.Alikimbizwa hospitali mara moja kupata matibabu zaidi.
Zaidi ya watu 5,500 wamethibitishwa kufariki kutokana na janga hilo.
Wengi wa wanavijiji wangali wanasubiri misaada ya chakula na maji safi ya kunywa huku mashirika ya kutoa misaada ya kisema huenda ikachukua siku nyengine 5 kabla ya kuwafikia baadhi yao kutokana na kuharibiwa kabisa kwa miundo mbinu.
Umoja wa mataifa umetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuendelea kutoa misaada wakikadiria michango inayohitajika kuwa zaidi ya dolla millioni 415 kuisaidia Nepal katika kipindi cha miezi 3 ijayo.
No comments:
Post a Comment