Manchester United itakuwa nyumbani Old Trafford Jumapili hii kumenyana na Man City katika mchezo wa Manchester ‘derby’, vita inayotajwa kuwa kali kutokana na timu zote kusaka nafasi ya pili ili kuifukuzia Chelsea kileleni kwenye msimamo.
KOCHA Mkuu wa Manchester United, Louis van Gaal ametamba kwamba kupanda kiwango kwa kikosi chake kumeanza kuwatia presha mahasimu wao, Manchester City katika mbio zao za kusaka ubingwa wa Ligi Kuu England.
Manchester United itakuwa nyumbani Old Trafford
Jumapili hii kumenyana na Man City katika mchezo wa Manchester ‘derby’,
vita inayotajwa kuwa kali kutokana na timu zote kusaka nafasi ya pili
ili kuifukuzia Chelsea kileleni kwenye msimamo.
Kocha Van Gaal ameiongoza Man United kushinda
mechi tano zilizopita kwenye ligi na kupanda kwenye nafasi za juu katika
msimamo wa ligi ikishika nafasi ya tatu kabla ya mchezo wa jana
Jumatatu usiku kati ya Man City na Crystal Palace.
Mdachi huyo alisema mastaa wake kwa sasa
wanajiamini na wataendelea kutumia mbinu walizotumia katika kuzichapa
Liverpool na Tottenham wakati watakapokipiga na Man City.
“Ndiyo wachezaji wapo vizuri na wana hamasa zaidi na tunatazama pia aina ya wapinzani tunaowakabili,” alisema Van Gaal.
“Kwa sasa tunajiamini zaidi, hivyo timu yoyote
iliyo juu yetu ikipoteza pointi hilo litakuwa pigo kwao. Nadhani kiwango
chetu cha sasa hata Man City watakuwa wanakiogopa.”
Mchezo wa raundi ya kwanza kwenye Ligi Kuu
uliofanyika Etihad baina ya timu hizo, Man United ilikubali kichapo cha
bao 1-0, straika Sergio Aguero akiwatesa wababe hao wa Old Trafford.
No comments:
Post a Comment